Vera Sidika apanga kuboresha matiti yake

Muhtasari
  • Mkewe mwanamuziki Brown Mauzo alifunguka vya kutosha kuwafahamisha mashabiki wake kwamba hajisikii vizuri na mwili wake kufuatia kujifungua kwake hivi majuzi
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Video vixen,mjasiriamali na mwanasosholaiti Vera Sidika anapanga kuboresha matiti yake ambayo tayari ni ya kupandikiza.

Mama wa mtoto mmoja alichapisha  habari hizo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Vera alifichua kuwa ananuia kufanya ‘kazi ya kuchekesha’ hivi karibuni. Mkewe mwanamuziki Brown Mauzo alifunguka vya kutosha kuwafahamisha mashabiki wake kwamba hajisikii vizuri na mwili wake kufuatia kujifungua kwake hivi majuzi.

Hili lilikuwa ni jibu kwa mmoja wa washabiki wake ambaye alilalamika kuhusu kutoweka picha zake kwenye instagram.

Vera pia aliendelea kutoa ushauri kwa shabiki mmoja mahususi ambaye aliuliza ili kujua maoni yake ni nini kwa mtu anayechukua vipandikizi vya matiti.

"Siwezi kumshauri mtu yeyote jinsi ya kuishi maisha yake. Ninachoweza kusema ni ikiwa unaipenda, endelea nayo. Fanya kile kinachokufurahisha! Vipandikizi vya matiti ni salama! & mtu bado anaweza kunyonyesha kwa nini asinyonye,"alijibu.