Nitakupenda milele,'Kajala amwambia Harmonize baada ya kumvisha pete ya uchumba

Muhtasari
  • Hafla hiyo ilifanyika siku ya Jumamosi ambapo ilihudhuiwa na marafiki, familia na watu mashuhuri
Harmonize na Kajala
Harmonize na Kajala
Image: HISANI

Ni furaha kwa mwanamuziki na staa wwa bongo Harmonize baada ya mwigizaji na mpenzi wake Fridah Kajali kukubali pete yake ya uchumba.

Hafla hiyo ilifanyika siku ya Jumamosi ambapo ilihudhuiwa na marafiki, familia na watu mashuhuri.

Wapenzi hao wamekuwa wakivuma mitanddaoni kwa miezi sasa, ii ni baada ya Harmonize kujitokeza hadharani na kuamua kumuomba Kajala msamaha kwa kumkosea.

Harmonize alijaribu vyovyote awezavyo ili kupokea msamaha wa Kajala, na hatimaye aliweza kumsamehe.

Baada ya kumsamehe wawili hao wameonekana kujivinjari pamoja huku mapenzi yao yakionekana kunoga kila siku.

Kajala alimpa ahadi msanii Harmonize baada ya kumvisha pete ya uchumba na kusema kuwa;

"Rajabu... Nitakupenda Leo, Kesho, Hadi Milele,"Alisema Kajala.

Kutoa kwetu wanajambo hongera Kajala na Harmonize.