Nilifanya mapenzi na binamu zangu wengi kabla ya kuokoka- Kabi Wajesus afunguka

Kabi alisema visa vingi vya yeye kulala na binamu zake vilitokea kabla hajaokoka.

Muhtasari

•Kabi alikiri kuwa binamu yake aliyejitokeza mwaka jana kufichua kuwa wana mtoto pamoja sio pekee ambaye aliwahi kulala naye.

• Kabi pia alifichua kuwa alinyanyaswa na baadhi ya wanafamilia wake wakati alipokuwa anakua kijijini kwao.

amekiri kuwa aliwahi kulala na binamu zake wengi
Mwanavlogu Kabi Wajesus amekiri kuwa aliwahi kulala na binamu zake wengi
Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Mwanavlogu Peter Kabi almaarufu kama Kabi Wajesus amekiri kuwa amewahi kushiriki mapenzi na binamu zake kadhaa.

Alifichua hayo mbele ya waumini waliokuwa wamejumuika katika kanisa moja kwa ibada ya kesh iliyofanyika wikendi.

Kabi alikiri kuwa binamu yake ambaye alijitokeza mwaka jana kufichua kuwa wana mtoto pamoja sio pekee ambaye aliwahi kulala naye.

"Wengi wenu mnajua kilichofanyika mwaka jana. Kulikuwa na tukio la binamu yangu ambaye alijitokeza kusema tulilala naye na tuko na mtoto. Wengi wenu walishangaa kuwa nililala na binamu yangu," Kabi alisimulia.

Baba huyo wa watoto watatu alieleza kuwa visa vya yeye kulala na binamu vilifanyika kabla ya kupiga gatua ya kuokoka.

"Kabla sijaokoka, hilo halikuwa suala. Hakuwa wa kwanza, nilikuwa nimelala na wengine wengi. Huyu mwenye alipata mimba ndio tu mnajua," Aliongeza.

Mapema mwaka jana binamu ya Kabi anayetambulika kama Shiko alijitokeza kudai kwamba wana mtoto pamoja.

Awali mwanavlogu huyo alikuwa amekana madai hayo ila baadae akakiri kuwa ni kweli yeye ndiye baba ya bintiye Shiko. Hii ilikuwa baaada ya vipimo vya DNA kuthibitisha kuwa kwa kweli kuwa binti huyo mwenye umri wa miaka 8 ni wake.

"Ningetaka kudhibitisha kuwa matokeo ya DNA yalitolewa na kubaini kuwa mimi ndiye baba mzazi wa mtoto. Matokeo yanathibitisha kuwa, mnamo 2013 (ambayo ilikuwa kabla ya kuokoka na kuoa), nilimpata Abby"Kabi alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram mwezi Mei 2021.

Mwanavlogu huyo alishambuliwa sana mitandaoni baada ya kukiri hayo. Novemba mwaka jana Kabi alimtambulisha bintiye hadharani kupitia mitandao ya kijamii.

Katika ibada iliyofanyika Wikendi , Kabi pia alifichua kuwa alinyanyaswa na baadhi ya wanafamilia wake wakati alipokuwa anakua.

"Kitu kilitokea baina ya wazazi wangu ikabidi niende ushago. Watoto  walikuwa wananicheka kwa sababu ya Kikuyu yangu. Nilipoenda ushago baadhi ya wanafamilia wangu walichukua fursa kuninyanyasa," Alisimulia.