Jinsi Harmonize alivyotumia $58,000 kumwomba mchumba wake Frida Kajala msamaha

Kukununulia magari haya ni kwa sababu nakumbuka uliwahi kuniambia kuwa ni gari la ndoto zako

Muhtasari

•Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali maarufu kwa jina la Harmonize hakujua kuwa uhusiano wake na mwigizaji Frida Kajala utamgharimu mamilioni.

•Mnamo Aprili aliweka bango lililokuwa na Kajala akimsihi arudi. Pia aliingia kwenye mitandao ya kijamii akishiriki picha yake akiwa ameshika shada la maua mekundu akidai kumpenda Kajala akinukuu; “Nakupenda Kajala, naomba penzi lako tena.”

Harmonize na Kajala Masanja
Harmonize na Kajala Masanja
Image: HISANI

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali maarufu kwa jina la Harmonize hakujua kuwa uhusiano wake na mwigizaji Frida Kajala utamgharimu mamilioni.

Mnamo Aprili aliweka bango lililokuwa na Kajala akimsihi arudi. Pia aliingia kwenye mitandao ya kijamii akishiriki picha yake akiwa ameshika shada la maua mekundu akidai kumpenda Kajala akinukuu; Nakupenda Kajala, naomba penzi lako tena.”

 Kulingana na Alliance Media, kampuni ya matangazo ya nje ambayo inafanya kazi nchini Kenya na Tanzania, bango la mita 10 kwa mita 12 hugharimu takriban TSh4.6 milioni ($1,972) kwa mwezi, na malipo ya ziada ya uchapishaji ya TSh2.7 milioni ($1,157). Tsh230,000 ya ziada ($98) inatozwa kwa usakinishaji.

"Bei zetu kwa kawaida ni sawa bila kujali eneo na tunatoa arubuni kulingana na muda," Ramla Mbuya kutoka Alliance media alisema.

Alipoona kwamba bango hilo halizai matunda mengi, alitangulia kununua gari aina ya Evoque nyeusi na nyeupe yenye namba maalum zenye jina la mwigizaji huyo.

“Hata angekuwepo Kajala 1 hadi 10 hawawezi kufuta maumivu niliyokusababishia wewe na familia yako. Haiwezi kubadilisha tuliyopitia au kuwa sababu ya wewe kurudi kwangu. Inaeleza tu jinsi ninavyojutia maumivu niliyokusababishia. Kitu pekee ninachoomba kwako ni msamaha. Nataka ujue kuwa ninakupenda kwa moyo wangu wote, nipe tu nafasi nyingine. Sababu ya kukununulia magari haya ni kwa sababu nakumbuka uliwahi kuniambia kuwa ni gari la ndoto zako,” Harmonize alisema.

Smart Integrated Solutions International (SISI) Limited, kampuni ya uuzaji wa magari nchini Tanzania, inakadiria Range Rover Evoque kuwa TSh70 milioni ($30,017).

“Wewe ni mmoja wa wanawake hodari ambao nimewahi kuwaona katika maisha yangu, umekuwa kwa ajili yangu. Kuna wakati sikuwa hata na nyumba ya kulala lakini ulinipa sehemu ya kukaa. Yote tuliyopitia pamoja yamenifanya nitambue kuwa wewe ni mwanamke wa maisha yangu,” Harmonize alisema wakati wa hotuba yake ya pendekezo.

Mbali na hayo yote alimteua Mkurugenzi Mtendaji wa lebo yake ya muziki ya Konde Gang. Kajala pia atakaimu kama meneja wa Harmonize, akisimamia masuala yake ya muziki.