Ringtone Apoko afunguka jinsi wasichana walivyochochea uamuzi wake kugura injili

Alitangaza kuwa sasa atakuwa anaachia nyimbo za mapenzi baada ya kuipa kisogo tasnia ya injili

Muhtasari

•Ringtone alidai kwamba alijiondoa kwa kuwa angetaka kuona wasichana wakimuangazia Yesu badala ya yeye.

•Alitangaza kwamba sasa atakuwa anaachia nyimbo za mapenzi baada ya kuweka kuipa kisogo taaluma yake ya muziki wa injili.

Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Mwimbaji Alex Apoko almaarufu Ringtone amedai kuwa wanawake wamechangia uamuzi wake kugura injili.

Akiwa kwenye mahojiano na Mpasho, Apoko alieleza kwamba alichukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mashabiki wake wengi wa kike walikuwa wakimuangazia yeye badala ya kufuata injili aliyoimba.

Alidai kwamba angetaka kuona wasichana wakimuangazia Yesu ndio maana akajiondoa kwenye tasnia ya injili.

"Naimba alafu wale wasichana ambao wananipenda wananifuata mimi badala wafuate Yesu. Nataka break kidogo. Nataka wasichana wamuangazie Yesu waachane na mimi," Ringtone alisema.

Msanii huyo ambaye amekuwa akiimba nyimbo za injili kwa zaidi ya mwongo mmoja alijigamba kuwa anamezewa mate na kundi kubwa la wanadada.

Alitangaza kwamba sasa atakuwa anaachia nyimbo za mapenzi baada ya kuweka kuipa kisogo tasnia ya injili.

"Wiki ijayo natoa wimbo wa kwanza wa mahaba. Sitaki kuwaweka mashabiki sana. Tayari nishafanya wimbo ambao unaitwa 'mapenzi yetu pamoja'," Alisema.

Aidha mwanamuziki huyo alipuuzilia mbali madai kuwa aligura injili kwa minajili ya mapato ya kifedha.

Ringtone alibainisha kuwa tayari amejizolea utajiri mkubwa kutokana na kazi yake ya muziki wa injili.

"Niko na pesa nyingi. Hata naweza nikafadhili sekta ya muziki wa kidunia ya Kenya. Naweza wafadhili wote. Siwezi kuenda huko kwa sababu ya pesa," Alisema.

Msanii huyo asiyepungukiwa na drama pia aliwatambua baadhi ya wanamuziki wa nyimbo za kutumbuiza wakiwemo Otile Brown, Diana B, Nadia Mukami na Willy Paul ambao atakuwa anaunga nao. 

"Wasihisi kama kwamba wanatishiwa," Alisema.

Ringtone alitangaza kuondoka kwake kwenye tasnia ya injili siku ya Jumatatu baada ya kuwa pale kwa takriban miaka 13.

Siku ya Jumanne alitangaza kwamba sasa atakuwa anatengeneza nyimbo za mapenzi na kuwaomba