"Pacha wangu!" Mamake Diamond amsherehekea baby mama wa Rayvanny

Wawili hao walizaliwa siku kama ya leo lakini miaka tofauti ya mbali.

Muhtasari

•Huku akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake Mama Dangote alimshukuru Mola kwa kumjalia uhai hadi wa leo.

• Fahyvanny kwa upande wake alisema anavuka daraja kuingia kwa umri mpya akiwa mtu mwenye furaha.

Mama Dangote na Fayvanny
Image: INSTAGRAM

Mama Dangote na aliyekuwa mpenzi wa Rayvanny, Fahyma almaarufu Fayvanny wanaadhimisha siku yao ya kuzaliwa.

Wawili hao walizaliwa siku kama ya leo lakini miaka tofauti ya mbali.

Huku akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake Mama Dangote alimshukuru Mola kwa kumjalia uhai hadi wa leo.

"Happy birthday kwangu...Kibibi Kizee kama anavyo niita Taraaj...🙏 Nashukuru Mungu kwakudizi kunipa pumzi mpaka hii leo. Alhamdulillaah," Mama Dangote alisema kupitia Instagram.

Mamia ya wanamitandao wamechukua fursa hiyo kumtakia kheri njema za siku ya kuzaliwa mama huyo wa Diamond.

Fayvanny ni mmoja wa ambao wamechukua hatua ya kumsherehekea mshirika huyo wake wa siku ya kuzaliwa.

"Happy Birthday mama yangu, nakupenda @mama_dangote," Aliandika Fayvanny kwenye Instastori zake.

Mama Dangote alionekana kupendezwa na ujumbe huo mtamu wa Fayvanny na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Pacha wangu, nakupenda sana @fayvanny," Mamake Diamond aliandika kwa screenshot ya Instastori ya baby mama huyo wa Rayvanny.

Huku akijisherehekea Fahyvanny alisema anavuka daraja kuingia kwa umri mpya akiwa mtu mwenye furaha.

Alipakia picha zake nyingi na kujiandikia jumbe nzuri huku mamia ya watu wakichukua fursa kumtakia kheri za siku ya kuzaliwa.

"Picha ni nyingi sana, hii birthday inaende hadi tarehe 20 mwezi huu, simalizi leo," Aliandika kwenye Instastori.

Baby mama wa Diamond, Hamisa Mobetto pia alimsherehekea Fayvanny.

"Kheri njema za siku ya kuzaliwa baby wangu @fayvanny,"

Mungu awajalie maisha marefu Mama Dangote na Fahyma wanapovuka kwa hatua mpya ya maisha yao.