"Imba, watu wanataka uimbe, si kupiga kelele na kuruka sarakasi," Mwijaku amponda Diamond

Diamond alitumbuiza katika tamasha la Afro Nation nchini Ureno wikendi iliyopita.

Muhtasari

• Mwijaku alizidi kumponda Diamond kwa kusema kwamba mitindo yake ya densi huwa anahariri.

Mwijaku, Diamond Platnumz
Mwijaku, Diamond Platnumz
Image: Instagram

Mtangazaji mwenye utata mwingi kutokea Tanzania, Mwijaku amemponda msanii Diamond Platnumz na kuikashfu jinsi alivyocheza kwenye tamasha la Afro Nation nchini Ureno, tamashac ambalo lilikuwa limejaa mastaa wa muziki kutoka nchi nyingi za Afrika magharibi na kusini.

Msanii Diamond Platnumz ndiye alikuwa msanii pekee kuwakilisha ukanda mzima wa Afrika mashariki katika ukumbi wa Algarve nchini Ureno.

Kusema kweli msanii Diamond alitisha pakubwa na kutikisa baada ya kupiga bonge la show ambayo haijapata kutokea msanii mwingine kutoka ukandaa huu wa kumlinganisha naye.

Watu mbali mbali walimpongeza sana kwa kuiwakilisha Afrika Mashariki, akiwemo Mwijaku , lakini inaonekana mtanagzaji huyo amekengeuka ghafla na kumponda kwa kusema kwamab hakuna cha ziada alichokifanya jukwaani zaidi ya kuruka ruka tu kama Mmaasai na shuka lake jekundu.

Mwijaku alisema kwamba msanii Burna Boy ndiye msanii aliyetikisa kikweli kwa kuimba na kumtaka Diamond anapopanda jukwaani awe anaimbia watu na wala si kucheza cheza densi, densi ambazo Mwijaku anasema Diamond huwa anahariri. Mwijaku alikuwa akimponda Diamond kwa jina la Mwamino.

Mwijaku alipakia video ya Burna Boy akimsifia huku akisema kwamab hiyo ndio show na Diamond anafaa kujifunza kutoka kwake.

“Tofauti ya kuimba na kuwafokea watu ili wapige kelele..! Huyu hapa ni ma boy @burnaboygram . NYOKO MWAMBINO. Mwambieni MWAMBINO MPUMBAVUUU KABISA AKIMHARIRI ZAKE TUNAZIJUA . Show hii hapa,” aliandika Mwijaku.

Katika tamasha hilo, baadhi ya wasanii waliimba alasiri huku magwiji wakiimba katika kilele cha tamasha lenyewe ambalo lilifanyika usiku. Diamond ni miongoni mwa wasanii waliopanda jukwaani alasiri na kufanya kile wazungu wanaita ‘curtain raising’. Mwijaku alitumia kigezo hicho na kumponda pakubwa Diamond ambapo alisema yeyote mwenye alipewa nafasi ya kutumbuiza jukwaani majira ya mchana hajatosha mboga.

“WALIO IMBA MCHANA WOOTE NI WATOTO MSISAHAI VILEEEE TUNAFANYAGA,” aliandika Mwijaku akionekana kumshambulia Diamond.

Mtangazaji huyo mwenye utata amekuwa akikanganya wengi hadi kushindwa kueleweka anasimama upande gani baina ya Diamond na wabaya wake kina Harmonize na Alikiba kwa sabqabu muda mwingi anaonekana kumponda Platnumz na kuwasifia Alikiba na Harmonize huku akiwa bado anaramba dili za ubalozi Wasafibet inayomilikiwa na Diamond.