“Alinizawadia milioni 20" Mama Dangote afichua kitu Diamond alimpa kama zawadi ya 'birthday'

Mama Dangote alikuwa anasherehekea miaka 54 ya kuzaliwa.

Muhtasari

• Diamond ambaye alikuwa nje ya nchi alimpa kiasi hicho cha pesa kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.

• Alikanusha madai kwamba yeye na Zuchu hawaonani na kusema mwanamuziki huyo pia alimpigia simu na kumsherehekea.

Mama Dangote na mwanawe Diamond Platnumz
Mama Dangote na mwanawe Diamond Platnumz
Image: Instagram

Bi. Sandra ambaye wengi waanmfahamu kama Mama Dangote, mama wa kumzaa mwanamuziki nguli kutokea Tanzania, Diamond Platnumz amefichua kiasi cha hela ambacho Diamond alimzawidia siku yake ya kuzaliwa ambayo ilifanyika juzi.

Katika hafla hiyo ambayo mwanawe, Esma Platnumz alimuandalia pasi na ufahamu wake, kwa kimombo ‘surprise’ mama Dangote alisema kwamba bintiye alimpigia simu na kumtaka afike kwake ambapo kwa mshangao mkubwa alipata ameandaliwa bonge la hafla ambapo kila mtu alikuwa akimuimbia nyimbo za kheri njema zilizokuwa zimehanikiza katika janibu zote za mbali na karibu ya maeneo yale.

Alisema kwamba Diamond ambaye bado yupo nje ya nchi alimpigia simu kumtakia kheri njema na kumuuliza ni zawadi gani nzuri ambayo angependa kumpa, Mama Dangote alisema aliambiwa mwanawe kwamba hakuwa na mpango wowote.

Diamond aliingia kwenye akiba ya mtoto wa kiume na kumrushia zawadi ya elfu milioni ishirini pesa za Kitanzania ambacho ni kiasi sawa na milioni moja na ushehi pesa taslimu za benki kuu ya Kenya.

“Amenizawadia milioni 20, naona ni zile alikuwa anataka kunipa ili nitoke kujivinjari nazo,” alisema Mama Dangote.

Bi. Sandra alikuwa akisherehekea miaka 54 ya kuzaliwa kwake ambapo wanawe walijichanga na kurusha bonge la ‘party’ ambayo imesalia kuzungumziwa na wengi si kwenye vyombo vya habari, si mitandaoni, si vijiweni, kila mahali.

Kukosekana kwa msanii Zuchu kwenye hafla hiyo kulizua minong’ono mitandaoni ambapo baadhi walizua kwamba Mama Dangote hamtaki Zuchu kwa kile kinachosemekana kwamba mwanawe Diamond tayari yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Zuchu.

Mama Dangote alikanusha madai hayo na kusema kwamba Zuchu mwenyewe alimpigia simu asubuhi ya siku ya kusherehekea na kumtakia kila la kheri ambapo pia alimtaka atoke kwa ajili ya kujivinjari.

Ikumbukwe mwanamuziki Zuchu kukosekana kwake kweney hafla ile hakukuwa maksudi kama ambavyo wengi walikuwa wakisema kwani yuko nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya video ya ngoma zake mpya ambazo ameziachia hivi karibuni na zimekuwa zikifanya vizuri sana kweney majukwaa mbalimbali ya kupakua miziki licha ya kuwa bado video rasmi hazijatoka.