Frida Kajala hatimaye afichua kwa nini anampenda Harmonize

Kweli, watumiaji mitandao kadhaa wa mtandao hawakukubaliana na matamshi na ufichuzi wake Kajala.

Muhtasari
  • Frida Kajala hatimaye afichua kwa nini anampenda Harmonize
  • Mwigizaji  huyo aliibua hisia kutoka kwa wafuasi wake mtandaoni ambao hawakusita kutoa mawazo yao.
mnamo siku ya kuvisha pete ya uchumba
Harmonize na Kajala mnamo siku ya kuvisha pete ya uchumba
Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Mwigizaji kutoka Tanzania, Frida Kajala amechapisha chapisho kwenye mitandao yake ya kijamii  na kufichua umma kwa nini anampenda mchumba wake, Harmonize.

Mama huyo wa mtoto mmoja alifichua hayo baada ya kuweka picha ambayo walipiga kwenye sherehe ya uchumba wao.

Wanandoa hao ambao walirudiana hivi majuzi baada ya kuachana kwao wamekuwa wakijulikana kwa muda sasa. Hii ni tangu Harmonize amchumbie Kajala.

Kajala alishiriki picha kwenyeukurasa wake wa Instagram kisha akaendelea kufichua kwa nini anapenda harmonize.

Mwigizaji  huyo aliibua hisia kutoka kwa wafuasi wake mtandaoni ambao hawakusita kutoa mawazo yao.

Frida alieleza waziwazi kwenye chapisho hilo sababu inayomfanya kumpenda Harmonize. Alidai kuwa anampenda kwa sababu watu wanawapinga.

Kweli, watumiaji mitandao kadhaa wa mtandao hawakukubaliana na matamshi na ufichuzi wake Kajala.

"Nampenda kwa sababu dunia nzima inatupinga", Kajala alifichua.