Wig zangu zikinuka ni zangu-Manzi wa Kibera amwambia aliyekuwa mpenziwe Stivo Simple Boy

Sasa habari hii kuhusu Manzi Wa Kibera akimshutumu Pritty kwa kumkejeli imeenea mtandaoni ambapo, inazua hisia tofauti kwa sasa.

Muhtasari
  • Sasa habari hii kuhusu Manzi Wa Kibera akimshutumu Pritty kwa kumkejeli imeenea mtandaoni ambapo, inazua hisia tofauti kwa sasa
Manzi wa Kibera
Image: Hisani

Manzi Wa Kibera ameibua hisia kwenye mitandao tofauti ya kijamii. Hii ni baada ya kumshutumu Pritty Vishy kwa kumkejeli, jambo ambalo Wakenya hawawezi kuacha kulizungumzia kwenye mitandao tofauti ya kijamii.

Kulingana na picha ya skrini ambayo inazunguka mtandaoni kwa sasa, Manzi Wa Kibera alikuwa na uchungu kwa Pritty ambapo alisema, wig zake huwa zinanuka.

Sasa habari hii kuhusu Manzi Wa Kibera akimshutumu Pritty kwa kumkejeli imeenea mtandaoni ambapo, inazua hisia tofauti kwa sasa.

Wengi wako tayari kuwaambia wanawake hao wawili wasuluhishe mizozo yao huku wengine wakiwa nje wakimuuliza Pritty ikiwa Manzi Wa Kibera anasema ukweli kuhusu yeye kwa wakati mmoja.

"Na mtu asinitaje taje ata kama wig zangu zinanuka ni zangu, unasema Stivo Simple Boy hawezi ilhali ni yeye amefanya utambulike mitandaoni,mimi huwa nachapa watu,tunaishi sehemu tofauti KIbera."Manzi wa KIbera alimuonya Pritty.

Sio mara ya wanza kuona watu mashuhurri wakipondana mitandaoni kwani tumeshuhudia wengi wakikejeliana mitandaoni, huku baada ya muda ikiibuka kuwa walikuwa wanatafuta kiki

Haya basi wacha tuone kama wawili hawa wanatafuta kiki au la.

Una lipi la kusema kuhusu Manzi Wa Kibera akimshutumu Pritty kwa kumponda?