"Uchumi umepanda, acha kumtolea Mungu 10%, ongeza kiwango!" Mchungaji awarai waumini

Mchungaji huyo alisema uchumi umepanda na vitu viko juu na hivyo kuwataka waumini pia kuongeza fungu lao kutoka kumi hadi 70%

Muhtasari

• Baada ya watu kumchemkia, alijirudi na kusema maneno yake yalinukuliwa vibaya.

• Alisema yeye hutoa 70% kwa sababu mambo yako juu na uchumi uko juu zaidi.

Mchungaji Gospel Agochukwu aliwataka waumini kukoma kumtolea Mungu 10% na badala yake kuongeza kwani uchumi umepanda
Mchungaji Gospel Agochukwu aliwataka waumini kukoma kumtolea Mungu 10% na badala yake kuongeza kwani uchumi umepanda
Image: Facebook///Gospel Agochukwu

Mchungaji mmoja kutoka nchini Nigeria kwa jina Gospel Agochukwu amekuwa kioja cha kuzungumziwa mitandaoni baada ya kupakia ujumbe kwenye Facebook yake akiwataka waumini kuzidisha kiwango cha sadaka ya fungu la kumi hadi asilimia 70.

Mchungaji huyo alisema kwamba uchumi umedorora sana na kwa sababu kila kitu kimepanda bei basi ni vyema kwa waumini kuzidisha sadaka hiyo kutoka kiwango cha 10% ambacho biblia inasema hadi kiwango cha 70%.

“Uchumi ni mbaya, kila kitu kimepanda bei. Acha kumtolea Mungu 10%,” aliandika mchungaji Gospel Agochukwu.

Ujumbe huu kwa waumini ulipokelewa kwa njia tofauti tofauti huku wengi wakionekana kutofautiana naye hadi wengine kutishia kuasi ibada na kanisa kwa jumla.

Hii ilimlazimu mchungaji huo kurejelea ujumbe wake na kusema kwamba watu wengi walimzomea na kumkomalia walielewa vitofauti ujumbe huo na kusema kwamab alikuwa na maana kwamba uchumi umepanda lakini hakuna kitu katika nyumba ya bwana ambacho kimebadilika.

“Post yangu ya Mwisho kwenye 'UCHUMI NI MBAYA ONGEZA FUNGU LAKO' Ilieleweka vibaya na idadi kubwa ya watu, Nilikuwa najaribu kusema uchumi wa taifa ni mbaya na kila kitu ni ghali lakini hakuna kitu katika nyumba ya Mungu kimepanda kwa hivyo kanisa ndio uchumi pekee unaostawi nyakati kama hizi. Na watu wanapaswa kulipongeza kanisa kwa hilo,” mchungaji Gospel Agochukwu alibadilika ghafla kama lumbwi kwa kutetea kauli yake.

Mchungaji huyo aliweka wqazi na kusema kwamba hata hivyo hababaishwi na mzomo wowote na kuomba radhi kwa wale wote ambao waliupokea ujumbe huo kwa njia isiyoeleweka.

“Hata hivyo nakubali kila lawama, matusi na mitazamo kinyume na ninaomba radhi kwa wale ambao huenda wamechanganyikiwa kwenye suala la zaka na sikusudii kumkosea mtu tafadhali mnisamehe kama hamkunielewa vizuri. Biblia ilisema 10% lakini huwezi kulazimishwa au kubanwa kutoa. Mitume walitoa vyote walivyokuwa navyo... Suala hili linatofautiana kulingana na kiwango cha imani yako na uhusiano wa kibinafsi na Mungu,” alisema mchungaji Gospel Agochukwu kwenye ukurasa wake wa Facebook.