Alipoteza nywele kwa kansa, kijanake akalea nywele inchi 12 kwa miaka 3 ili kumuundia wigi

Melanie Shaha alipoteza nywele alipopewa matibabu ya kansa ya ubongo kwa njia ya mionzi ambapo upara ulianza kuingi.

Muhtasari

• Baada ya mionzi ya kuchoma saratani kuathiri mishipa ya kutengeneza nywele kichwani, Mekanie alianza kupoteza nywele.

• Kijana yake, Matt Shaha alijitolea kulea nywele kwa miaka 3 ili kumtengenezea mamake wigi la kufunika upara wake.

Matt Shaha na mamake Melenie Shaha aliyepoteza nywele kwa sababu ya saratani
Matt Shaha na mamake Melenie Shaha aliyepoteza nywele kwa sababu ya saratani
Image: Shaha Family

Mwanamke mmoja kutoka eneo la Arizona Marekani amehimiza watu wengi baada ya kufunguka hadithi yake jinsi alivyopoteza nywele kutokana na saratani ya ubongo lakini kijana wake akaamua kufuga nywele zake ili kumkabidhi kama mbadala.

Mama huyo alisema kwamab mtoto wake wa kiume alilea nywele zake kwa miaka kadhaa ili kumkabidhi kama wigi baada ya nywele zake halisi kupotea kutokana na saratani ya ubongo.

Melanie Shaha alianza kupata maumivu ya kichwa mwaka 2003 ambapo baadae madaktari walidhibitisha ni dalili za saratani ya ubongo, ugonjwa ambao ulisababisha nywele zake kukataa kuota kabisa na kichwa kuwa na upara.

Akizungumza na jarida moja la nchini humo kwa jina Today Parents, Shaha ambaye ni mama wa watoto sita alisema alijaribu kufanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe huo ila ikashindikana kwa mara ya kwanza, na pia mara ya pili mwaka 2006 akajaribu upasuaji mwingine bila mafanikio hadi mara ya tatu mnamo mwaka 2017 alipojaribiwa na mionzi.

Kulingana na jarida hilo, Shaha alimuuliza daktari iwapo angepoteza nywele zake na daktari akamhakikishia kwamba nywele hazingepotea ila miezi mitatu baadae akaanza kupoteza nywele na kuwa na upara asilimia kubwa ya kichwa baada ya kufanyiwa ukaguzi wa mionzi mwaka 2017.

Alipogundua anapoteza nywele, kijana wake kwa jina Matt Shaha siku moja wakila chamcha alizua wazo la kutaka kulea nywele zake ili kumfaidi mamake kama wigi la kubandika.

Kufikia mwezi wa tatu mwaka 2021, Matt alikuwa tayari amelea nywele zenye urefu wa inchi kumi na mbili ambazo walizikata na kupeleka kutengenezea mamake wigi la kichwani ambalo mpaka alipokuwa akifanya mahojiano yale alikuwa akilitumia kama nywele zake mwenyewe.