(Video) Mwanajeshi alemewa na hisia kukutana na wanawe baada ya miezi 10 vitani

Mwanajeshi huyo alikosa kuwepo wakati wa mchakato wa kuzaliwa mtoto wake mdogo na pia kukosa kuwepo mwanawe mkubwa akianza chekechea.

Muhtasari

• “Wakati huu muhali kutokea ulimfanya kujawa na hisia nzito baada ya kuwakumbatia wanawe mikononi mwake hatimaye,”

Wanasema kazi ya jeshini moja ya kazi ngumu sana duniani ambazo zinahitaji mtu kujitolea kwa moyo wote ili kuitumikia nchi yake mbali na watu wa karibu wa familia. Ni kazi ambayo inahitaji moyo mgumu na ujasiri uliopitiliza.

Video moja ambayo imepakiwa katika ukurasa mmoja wa Facebook kwa jina Humankind kutoka shirika la habari la US Daily ni moja ya kuelezea hisia kali za baba mwanajeshi aliyerejea nyumbani baada ya miezi kumi mbali na familia yake.

Katika video hiyo, mwanajeshi huyo anayetambuliwa kama sajenti Brown, alikuwa mbali na familia yake kwa zaidi ya miezi kumi ambapo alirejea baadae na kupata watoto wake wawili wote wa kiume wakiwa wamemsubiri kwa hamu kubwa.

Brown hakuwepo waakti mtoto wake mdogo anazaliwa na aliporejea huwezi amini jinsi machozi ya furaha yalimtoka watoto wake walipomkumbatia.

Video hiyo inaelezea hisia za baba kwa wanawe, watoto wakimzingira kwa furaha nyingi zinazofungulia mifereji ya machozi ya furaha kutoka machoni mwake.

“Mwanajeshi huyu amekaa mbali na familia yake kwa zaidi ya miezi 10 ambapo alikosa kuzaliwa kwa mwanawe mdogo na pia kukosa kuona mwanawe mkubwa akijiunga na chekechea,” maandishi kweney video hiyo yanaelezea tukio zima.

Kukosekana katika hatua muhimu za wanawe haswa ndiko kulisababisha mwanajeshi mkakamavu kulemewa na hisia, hisia ambazo zilidhihirika kupitia machozi ya furaha akiwakumbatia wanawe asiamini kama kweli ni yeye amepata kurejea nyumbani na kuiona familia yake ikiwa imesalimika muda wote alipokuwa mbali.

“Wakati huu muhali kutokea ulimfanya kujawa na hisia nzito baada ya kuwakumbatia wanawe mikononi mwake hatimaye,”

Video hiyo imewasisimua watu wengi huku baadhi wakitolea ushuhuda jinsi walivyohisi kurejea nyumbani baada ya kutengana na familia kwa muda mrefu na kusema kwamab haswa kazi ya jeshi ni ngumu mwanajeshi anaposalimika kurudi kwa familia yake akiwa hai basi huo huwa ni wakati wa kipekee katika maisha yake.

Video hiyo mpaka sasa imepata utazamaji wa zaidi ya watu laki na nusu.