Jimal Rohosafi ashauri akina dada Kujitegemea kifedha

Pesa za "Kumiliki" sio pesa ambazo mumewe humpa

Muhtasari

•Haijalishi mwanamke yuko katika hatua gani ya maisha, anahitaji pesa zake mwenyewe. Pesa za "Kumiliki" sio pesa ambazo mumewe humpa.

•Kuna vitu vingi ambavyo wanawake hupigana nazo kila siku. Ingawa wengi wamesalia kushinda, wengine wanashindwa.

 

Mfanyabiashara Jimal Rohosafi akionekana mwenye mawazo tumbi nzima
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi akionekana mwenye mawazo tumbi nzima
Image: Instagram//JimalRohosafi

Jamal rohosafi kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwashauri akina dada kufanya kazi kwa bidii ili wajitegemee kwa mahitaji yao ya kimsingi.

Aliendelea kudokeza kuwa kila mara akina dada wanapotaka pesa  za matumizi huwa wanajiingiza katika vitendo vya kuhushisha mwili wao kwa mnajili ya kupewa pesa.

''Wanawake wapendwa, fanyeni kazi kwa bidii ili mtakapohitaji Pizza, mfungue pochi zenu sio miguu zenu,'' Jimal alisema.

Kuna vitu vingi ambavyo wanawake hupigana nazo kila siku. Ingawa wengi wamesalia kushinda, wengine wanashindwa.

Si jambo la kawaida kupata wanawake wakizingatia kazi zao na kujisimamia wenyewe.

Haijalishi mwanamke yuko katika hatua gani ya maisha, anahitaji pesa zake mwenyewe. Pesa za "Kumiliki" sio pesa ambazo mumewe humpa.

Pesa "ya kumiliki" ni pesa inayofungamana na uhuru wa mwanamke na inatokana na kazi yake, uwekezaji na miradi mingine ya kujitegemea.

Watu wengi hukuwa na mtazamo hasi dhidi ya wanawake ambao wanaotoa kauli kama vile "Sihitaji mwanaume!" ilhali wanawake hao ndiyo wanaojua kwamba kujitegemea ni kitu muhimu sana.

Kwasababu ikiwa wanataka kuenda  safari nje ya nchi, wanauwezo wa kufanya hivyo.

Ikiwa wanataka kujinunulia nguo, begi nzuri au kwenda kula, wanaweza kufanya hivyo bila kuomba mwanaume pesa.

Mwanamke kama huyo, yuko huru kutenda jambo lolote bila kulazimika kuiuliza ama kujieleza kwa mwanaume sababu ya kufanya mambo mengine.

Jamal Roho Safi ni mwanabiashara ambaye  kupitia bidii yake amepata manufaa mengi haswa kutokana na biashara zake.