Ujumbe wa Ben Pol kwa mashabiki baada ya kumpoteza baba yake

Wikendi iliyopita Ben kupitia ukurasa wake wa instagram alitangaza kifo cha baba yake.

Muhtasari
  • HUku akiwashukuru mashabiki wake msanii huyo alisema kwamba huu ni wakati mgumu maishani mwake
msanii Arnelisa Muigai
Ben Pol msanii Arnelisa Muigai
Image: Instagram

Msanii maarufu kutoka Tanzania, Ben Pol amewashukuru mashabiki wake kwa kusimama naye wakati wa kipindi hiki kigumu.

Wikendi iliyopita Ben kupitia ukurasa wake wa instagram alitangaza kifo cha baba yake.

HUku akiwashukuru mashabiki wake msanii huyo alisema kwamba huu ni wakati mgumu maishani mwake.

Ujumbe aliopakia kwenye ukurasa wake wa instagram ulisoma;

"Asante sana kwa kutufikiria katika kipindi hiki kigumu, ushirikiano wako wa hali na mali, jumbe za faraja, ushiriki, simu, kututembelea vina maana kubwa sana kwetu na kamwe hatuwezi kusahau.Mwenyezi Mungu ampumzishe Mzee wetu mahala pema, nawe akuzidishie baraka.Kwa niaba ya familia ya Mzee Paul Mnyang’anga," Aliandika Ben Pol.

Msanii huyo hakufchua kilichosababisha kifo cha baba yake.

Ben aliwashukuru mashabiki wake na kusema kwamba hatasahau jumbe zao za kutia moyo.

"Siku hizi chache zilizopita zimekuwa ngumu. Asante kwa kutufanya tujisikie kuwa na msingi zaidi. Rambirambi zenu za fadhili zina maana zaidi kuliko mnavyojua. Mungu awabariki."