(+video) Bwana Harusi Mbilikimo Aibika Kucheza Densi Peke Yake Bi harusi Akiketi

Video hiyo ilipakiwa na ukurasa wa Gossip Mill kwenye Instagram

Muhtasari

• Video hiyo iiwaacha wengi katika gumzo kali kuhusu ni kwa nini bibi harusi aliamua kumuacha mumewe kucheza desni peke yake.

Video moja ambapo ilipakiwa kwenye mtandao wa Instagram inaonesha hafla ya harusi moja kati ya jamaa mbilikimo na mchumba wake mrefu.

Katika video hiyo na kile ambacho kimeifanya kusambazwa pakubwa ni kutokana na kwamba jamaa huyo mbilikimo anaonekana akijiachia mazima katika kusakata densi huku mchumba wake akiwa ameketi tu kama mtu ambaye hana haja na tukio zima katika hafla hiyo.

Video hiyo ilipakiwa na ukurasa wa Gossip Mill kwenye Instagram na tukio hilo liiwagawanya wanajamii ya mtandaoni katika makundi kadhaa baadhi wakisema wachumba hao waachwe wawe vile wanataka huku wengine wakizamia zaidi jinsi bibi harusi alivyokuwa ameketi bila kujali huku bwana harusi akijiachia kweli kweli katika densi peke yake.

Watu ambao wanaonekana kucheza na bwana harusi mbilikomo huyo ni wanaume wenzake huku bibi harusi akiwa amejiketia na kunong’onezana na watu wengine.

Mwingine alisema kwamba hao wanaume waliokuwa wakicheza densi na bwana harusi walikuwa wanamtania tu ila dhumni kuwa ni kulenga kuchepuka na mkewe.

“Lool huu ni uthibitisho kwamba wanaume na wanawake hawawezi kamwe kuwa sawa katika nyanja ya maoni ya jamii,” mmoja aliandika.

Wengine walimsifia bwaan huyo mfupi kwa kuenda nje ya vigezo vingi na kuhakikisha amepata mke licha ya dhana iliyopo katika jamii kuhusu watu wafupi kwamba wanawake wengi wanaibika kuchumbiwa na mbilikimo kutokana na kuogopa jinsi jamii itawachukulia au hata kuogopa kuzaa watoto ambao ni mbilikimo kama baba yao.