(+video) "Aliweka Picha Yangu Kama WhatsApp DP Yake, Hapo Ndio Nilipata Mchumba"

Mwanamke huyo alielezea jinsi rafiki yake aliweka picha yake kama dp ya WhatsApp na mumewe mtarajiwa akaomba nambake

Muhtasari

• "Winnie ahsante kwa kunipa mume wangu mtarajiwa" - mwanadada huyo alielezea.

Wachumba hupatana kwa njia mbali mbali, iwe ni katika matukio na nadra au katika hafla, lakini kwa mwanamke mmoja, kupata na mchumba wake kulikuwa tofauti kabisa kwani anaelezea kwamba alipatana na mchumba wake kupitia rafiki yake wa kike aliyetumia picha yake kama utambulisho wake kwenye mtandao wa WhatsApp, vijana wa mjini wanaita DP.

Katika video ambayo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, mwanamke huyo alielezea kwamba rafiki yake kwa jina Winnie alimuweka kwenye DP ya WhatsApp yake na mwanaume huyo ambaye sasa ni mumewe alimfuata W innie akamuambia angetaka kujua mwenye picha hiyo na hivyo ndivyo walivyokutana.

“Winnie aliniweka DP, kupitia ile picha ya profaili ya mwaka 2017 ndio mume wangu mtarajiwa aliponiona, moja kwa moja aliomba namba yangu ya simu. Winnie ahsante sana kwa kunipatia mume,” Mwanamke huyo alimshukuru rafikiye Winnie.

Pia alizidi mbele kusema kwamba mwanaume huyo ambaye sasa walikuwa waanfunga ndoa naye kipindi hicho akisimulia hayo hakua na nia ya kumchezea kwa sababu ujumbe wa kwamba alipopatiwa namba yake alimuambia nia yake ilikuwa ni kutaka kumujoa.

“Hakua na nia ya kunichezea, ujumbe wa kwanza aliniambia nataka nikuoe, mimi ndio sikuamini lakini leo kweli nimeamini,” alielezea huku watu wakishangilia.

Ama kweli kama fungu ni lako, litakufuata tu popote maana Mungu kesharidhia.