Amber Ray athibitisha kutengana na mpenzi wake Kennedy Rapudo

mama huyo wa mtoto mmoja alitaka kufafanua kuwa uhusiano wao haukufaulu kama alivyotarajia.

Muhtasari
  • Amber Ray athibitisha kutengana na mpenzi wake Kennedy Rapudo
Amber Ray
Image: Kwa Hisani

Mwanasosholaiti na mfanyabiashara Mkenya Amber Ray amethibitisha kwamba hayuko tena katika uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake Kennedy Rapudo.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, mama huyo wa mtoto mmoja alitaka kufafanua kuwa uhusiano wao haukufaulu kama alivyotarajia.

“Nop, najua mahali imefika naweza kuonekana mcheshi lakini manze sijui nifanyeje kama haifanyi kazi.....haifanyiki...so munipende tu vile niko,” aliandika.

Mfanyabiashara huyo hata hivyo hakueleza kwa undani kilichojiri kabla ya uhusiano kuisha.

Wapenzi hao wawili walianza kuchumbiana miezi miwili iliyopita baada ya Amber ray kuachana na mpenzi wake wa Sierra Leone na mchezaji wa mpira wa vikapu IB Kabba.