"Hawajafika kiwango cha 'Ni God manze'" KRA yasema haitatoza ushuru watoto walioajiriwa na mama yao

Ilisema kiwango cha mshahara wao ni kidogo na kutama umma kuwajulisha mshahara wao ukifika kiwango cha "Ni God manze"

Muhtasari

• “Tujulishe watakapofika kiwango cha mapato cha "Ni God Manze"” KRA iliwakata mbavu Watumizi wa Twitter.

Mamlaka hiyo ilisema haitawatoza ushuru watoto walioajiriwa kazi na mama yao
KRA Mamlaka hiyo ilisema haitawatoza ushuru watoto walioajiriwa kazi na mama yao
Image: the star

Juzi kati, mwanamke mmoja ambaye ni meneja wa rasilimali za watu kitaaluma kwa jina Kimoi Jerotich alizua bashasha mitandaoni baada ya barua zake za kuwaajiri wanawe wachanga kuvujishwa.

Kulingana na barua hizo, Jerotich alikuwa amewaajiri wanawe Shawn mwenye umri wa miaka 6 kufanya kazi ya kukusanya mayai ya kuku na kuyahifadhi sehemu salama huku ndugu yake Ryan wa miaka 9 akipewa kazi ya kunyunyizia shamba maji.

Kulingana na barua hiyo, Jerotich aliwaandikia vijana wake hao wachanga akiwaambia kwamba mshahara wao umeongezwa kutoka kiwango cha shilingi 20 kila Jumapili ya wiki hadi shilingi 30 baada ya kuwatathmini kwa miezi sita iliyopita na sasa mshahara wao wa kila mwezi utakuwa shilingi 120 za Kenya kwa kila mmoja.

jerotich
jerotich

Hili liliwafanya baadhi ya wakenya walioona barua hizo kuelekea kwenye mtandao wa Twitter na kuzua mjadala ambapo miongoni mwa mjadala huo wengi walitaja mamlaka ya ukusanyaji kodi KRA ili kuingilia kati na kuchukua tozo kutoka kwa wafanyikazi hao wachanga.

Baada ya mamlaka hiyo kutajwa kwa wingi na kutokana na inavyojulikana kujibu masuala mbali mbali kwenye mtandao wa Twitter, na kweli walijibu katika moja ya Tweet za ucheshi mno kama ilivyo kawaida yao.

Kwa upande wake, mamlaka ya KRA ilisema kwamba imeona hadithi hiyo ya waajiri wapya wasiotozwa na kusema kwamab kutokana na kiwango kidogo cha mshahara wanaopokezwa na mama yao, haitawezekana kwa mamlaka hiyo kuwaweka katika mpango wa kuchangia katika kutoa ushuru kwa taifa.

“Wanachopata ni chini ya mapato ya chini yanayotozwa ushuru,” KRA ilijibu hatimaye.

Pia mamlaka hiyo ilizidi kueleza kwamba itazidi kuwafuatilia vijana hao na kutama umma kuwajulisha pindi mishahara yao itakapofika kiwango cha juu ambacho Wakenya wengi waliofanikiwa wanapoulizwa hupenda kusema ni Mungu amewasaidia.

“Tujulishe watakapofika kiwango cha mapato cha "Ni God Manze"” KRA iliwakata mbavu Watumizi wa Twitter.