Kwa nini mwigizaji Njambi alikaa kwenye ndoa yenye unyanyasaji

Njeri anasema alidanganya mara nyingi kuhusu majeraha.

Muhtasari
  • Njambi anasema angedanganya ili kumlinda baba wa mtoto wake akitumai angebadilika. Akizungumza wakati wa mahojiano na Mungai Eve alisimulia

Njeri Gachomba kama vile anavyofahamika sana kwa jina lake la uigizaji Njambi akiwa kwenye mhojiano alifichua sababu ya kukaa kwenye ndoa ya unyanyasaji.

Hivi majuzi alimwacha baby daddy akisema ni mnyanyasaji na hana usalama sana.

Njambi anasema angedanganya ili kumlinda baba wa mtoto wake akitumai angebadilika. Akizungumza wakati wa mahojiano na Mungai Eve alisimulia;

" Siku moja nilienda kutembeana marafiki zangu na niliporudi simu yangu ilikuwa imezima.Niliporudi alidai na kuanza kutafuta ushahidi kwa sababu alidhani nilikuwa na mwanaume

Aliposhindwa kupata ushahidi alinipiga jicho na simu. Nilikuwa na jicho jeusi kwa mwezi mmoja."

Njeri anasema alidanganya mara nyingi kuhusu majeraha.

"Nilikuwa nimepangiwa mahojiano ya redio na ilibidi niende na vivuli. Mtangazaji wa redio aliniuliza mara kwa mara ikiwa ninanyanyaswa ili anitafutie msaada lakini nilipuuza,Nilijaribu kumlinda sana."

Alizidi kusimulia masaibu yake na kusema;

"90% yake alikuwa mzuri kwa hivyo nilifikiri ningeweza kukabiliana nayo. Kila alipokuwa akinipiga alikuwa akininunulia zawadi.

Sikuwahi kutaka kuwa single mother wa watoto wawili kwa hiyo ndiyo sababu nilibaki,Suala lilikuwa simu yangu kila wakati.

Ningepata kesi za kudanganya lakini siku zote nilimtetea kwa kusema yeye ni mwanaume.

Mara ya kwanza aliponipiga nilimwambia rafiki yangu wa karibu,Wakati mwingine alikuwa akiwapigia simu marafiki zangu huku akinipiga. Kila alipokuwa akinipiga alikuwa akinitishia kuniua au kuniharibu usoni."

Njambi anasema kuwa wakati fulani aliamua kuacha uhusiano huo kiakili kabla ya kuamua kuachana kabisa.