"Hapendi watu weusi!" Tanasha Donna amsuta jirani wa mamake mbaguzi wa rangi

Mzazi huyo mwenza wa Diamond alishangaa jinsi jirani huyo alivyomchagua farasi mweusi ilhali anawachukia watu weusi.

Muhtasari

•Jumatatu alipakia video inayoonyesha akiwa nje ya nyumba ya mamake na kufunguka kuhusu jirani wa mamake ambaye alimshtumu kwa kuwa mbaguzi wa rangi

•Mamake Tanasha, Bi Diana Oketch ni Mkenya kutoka jamii ya Luo ilhali baba yake ni mzaliwa wa Italia.

Image: INSTAGRAM// TANASHA DONNA

Mwanamuziki maarufu kutoka Kenya Tanasha Donna yuko nchini Ubelgiji ambako anafurahia wakati na mama yake.

Katika siku za hivi majuzi, mpenzi huyo wa zamani wa staa wa Bongo Diamond Platnumz amekuwa akitumia ukurasa wake wa Instagram kupakia picha na video zake akiwa katika nchi hiyo ya Ulaya.

Jumatatu alipakia video inayoonyesha akiwa nje ya nyumba ya mamake na kufunguka kuhusu jirani wa mamake ambaye alimshtumu kwa kuwa mbaguzi wa rangi

"Acha niwaambie kitu cha kushangaza. Jirani wa mamangu ni mbaguzi wa rangi waziwazi. Hapendi watu weusi na hata huwa hajaribu kuficha. Kila wakati familia ama marafiki wanapokuja huwa hajaribu kuficha," Tanasha Donna alisema katika video ambayo alipakia kwenye Instastori zake.

Mama huyo wa mvulana mmoja alifichua kuwa jirani huyo wa mamake hata hivyo anamiliki farasi mweusi.

Tanasha alishangaa jinsi jirani huyo alivyochagua kuwa na farasi mweusi ilhali anawachukia waziwazi watu weusi.

"Hupendi watu weusi lakini hujali kuwa na farasi mweusi. Huo ni upuuzi," Alilalamika.

Wiki iliyopita Tanasha alifichua kuwa yuko Ulaya ambako huwa anapenda kutembelea mara kwa mara na kubarizi na mama yake.

Mzazi huyo mwenza wa Diamond pia alitumia fursa hiyo kufunga ukweli kuhusu asili yake halisi.

"Watu wakiuliza ninatoka wapi huwa sijui nianzie wapi"

"Nilizaliwa Uingereza, nilikulia Kenya, kisha nikaondoka kwenda Ubelgiji, lakini baba wangu wa kibiolojia ni Muitaliano na mchanganyiko mwingine huko pia lakini alikua na baba wa kambo wa Ubelgiji, kisha nilirudi Kenya kama miaka 6/7 iliyopita. Huwa naenda na kurudi Ulaya/Kenya nitakapoweza" Alisema.

Hapo awali aliwahi kufichua kuwa mama yake hajawahi kupata fursa ya kukutana na mtoto wake na Diamond.

Mwimbaji huyo alipokuwa ameenda Dubai kwa likizo ya wiki moja  alisema kwamba ana mipango ya kubadilisha hilo.

“Nimempeza sana mtoto wangu, wakati ninapofanya ziara ya kikazi yuko shuleni na huwa na kazi nyingi sana shuleni, anapenda shule,” Alisema.

Aliongeza, "Ninapokuwa mbali naye, imekuwa siku tano sasa, ninahisi mtupu sana, nahisi kama kuna kitu kinakosekana. Kwa hivyo siwezi kusubiri kurudi kwake."

Tanasha akaendelea, "Mwajua mama yangu hajawahi kukutana na mwanangu? Sitaki kuanza kuchanganyikiwa na hii live sasa hivi. Lakini mama yangu hajawahi kukutana na mwanangu. Na anaenda kukutana naye kwa mara ya kwanza baada ya wiki tatu na nina furaha sana, itakuwa wakati wa kihisia sana kwangu na siwezi kusubiri."

Mamake Tanasha, Bi Diana Oketch ni Mkenya kutoka jamii ya Luo ilhali baba yake ni mzaliwa wa Italia.