(+video) Jinsi nilivyogundua mamangu ana ujauzito wa mume wangu - Vanessa

Mwanadada huyo alisema alivunjwa roho sana na mtu ambaye alikuwa anamaanisha kila kitu kwake - Mamake.

Muhtasari

• Baada ya kumwekea shinikizo mamake kwa simu, mamake alifunguka kwa kumpasulia mbarika kwamba amegundua ni mjamzito.

Katika maisha, kama umebahatika kuwa na mzazi, ndiye mtu wa mwisho kabisa unayeweza kufikiria kama atakusaliti.

Kwa mwanadada mmoja kwa jina Jules Vanessa, hadithi yake ni tofauti kabisa.

Vanessa katika msururu wa video ambazo alizipakia kwenye TikTok yake, aliwashangaza wengi alipoeleza kwa uchungu jinsi mama yake wa kumzaa alivyomsaliti. Kivipi?

Mama yake mzazi alichepuka na mpenzi wake, kwa maana kwamba mchumba wa Vanessa alikuwa anajihusisha kimapenzi na mamake na haikuishia hapo. Mama mzazi alimzunguruka mwanawe na kuzaa mtoto na mkwe wake.

Vanessa katika video hizo anaeleza kwamab alikuwa ameenda safari na marafiki zake na akiwa huko ziarani ndipo alimpigia mamake simu.

Kwa maelezo yake, sauti ya mamake ilikuwa kama ya mtu mwenye hajatulia na ndipo aliingiwa na wasiwasi zaidi kutaka kujua kama kila kitu kilikuwa sawa nyumbani.

Baada ya kumwekea shinikizo mamake kwa simu, mamake alifunguka kwa kumpasulia mbarika kwamba amegundua ni mjamzito.

Haikuishia hapo kwani Vanessa alitaka kujua ujauzito mamake kautoa wapi, kumbe hakujua jibu lilikuwa kama jipu litakalotumbuliwa usoni mwake na uzaha wote sekunde chache zilizofuata.

Mamake alimfungukia kwamba ujauzito ni wa mkwe, mchumba wa Vanessa!

Katika hali ya majonzi makubwa, Vanessa alieleza kwamab alishindwa la kufanya wala kusema na kujipata analowa kwenye bahari ya machozi huku akiwaachia karma kuwaadhibu katika muda wake sahihi.

“Nilikuwa ziarani na rafiki zangu na nikaamua kuwapigia simu wanawake wote katika maisha yangu. Kumpigia mamangu ghafla nikaskia analia, baada ya kumpigia tena ndio aliniambia kwamba ni mjamzito na ujauzito ni wa mchumba wangu,” Vanessa alieleza.