(+video) "Ukijua marupurupu yameingia!" Muuzaji acheza densi ya furaha mteja kununua gari

Alionekana akisakata densi kwa furaha huku akimkabidhi mteja funguo za gari.

Muhtasari

• Baada ya kumpokeza maua, kijana huyo anaamua kuyasindikiza kwa densi moja hatari, jambo lilalozua mihemko ya furaha mpaka mteja kujipata anasakata densi pia.

Hakuan kitu cha kuridhisha moyo na nafsi kama mjasiriamali kuona biashara yake inakua na mtaji kurudisha faida. Kwa wafanyikazi wauzaji, haswa wale wanaolipwa, furaha yao kuwa kubwa wanapoona mteja amefanya ununuzi kwa sababu hiyo ndio njia pekee ya kupata marupurupu yao.

Video moja inaonesha muuzaji akisherehekea kwa mbwembwe baada ya mteja kufanya ununuzi kwenye eneo lao la kuuza magari imewafurahish watu wengi katika mitandao ya kijamii.

Mhusika mkuu ni kijana mfanyikazi ambaye kazi yake ni kuwatongoza wateja ili kufanya ununuzi hapo alifurahia baada ya kumshawishi mteja mmoja mpakac kuhakikisha ameridhia kufanya biashara na kampuni hiyo.

Mteja huyo mwanamke mwenye umri wa makamo alinunua gari hapo na wafanyikazi wote wanaonekana kumshangilia kwa tabasamu, wengine wakichukua video huku kijana huyo mmoja akimpokeza maua na stakabadhi za gari.

Baada ya kumpokeza maua, kijana huyo anaamua kuyasindikiza kwa densi moja hatari, jambo lilalozua mihemko ya furaha mpaka mteja kujipata anasakata densi pia.

Video hiyo ilipakiwa kwenye mtandao wa Facebook na Phathutshedzo Sigudu Mutheiwana na maoni yalikuwa ya kuvunja mbavu.

“Wakati unajua kwamba marupurupu yanakuja,” Koreni Muremi aliandika.