Mwanamke achoma zawadi ya wigi aliyonunuliwa na mpenziwe kisa ni la bei rahisi (+video)

Baada ya kuliteketeza wigi hio, alitupa masalia yake kweney rundo la takataka.

Muhtasari

• “Siungi mkono upuuzi huu. Iwe feki au original jifunze kuwa appreciative maana hujui ilimchukua nini kununua hiyo" mmoja alisema.

Mwanamke mmoja amewaacha Watumiaji wa mitandao ya kijamii katika butwaa la karne baada ya video yake kuonekana akilichoma wigi alilonunuliwa na mpenzi wake kwa kudai kwamba ni la bei rahisi ikilinganishwa na hadhi yake.

Katika video iliyopakiwa kwenye Instagram na blogu ya Instablog9ja, mwanamke huyo inaarifiwa ndiye alipakia video hiyo akilichoma wigi hilo.

Baada ya kuliteketeza kwa moto, mwanadada alibeba mabaki na kutupa kweney rundo la taka nje ya nyumba yake.

Mwanamke mmoja, ambaye alifikiri kuwa mwanamke huyo alikuwa amemkasirikia mchuuzi aliyemuuzia wigi alimhimiza amfichue mchuuzi huyo wa nywele ili wengine waepuke mtu huyo.

Lakini alieleza kuwa mchuuzi hakufanya kosa lolote, bali ni mpenzi wake ndiye aliyempatia wigi kwa sababu hajui lile la ubora.

"Wewe kamtaje muuzaji  kwenye chapisho," shabiki mmoja aliyekuwa hajui kinachoendelea alimuambia.

"Muuzaji hajafanya lolote baya, bali ni mpenzi wangu amenighadhabisha kwa kuninunulia wigi la bei iliyokufa wakati hadhi yangu kubwa ya kifahari,” mwanadada huyo alieleza.

Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya wanamitandao kuona mwanamke huyo kama mtu asiye na shukrani ya kuridhika na kile kidogo alichopewa.

“Siungi mkono upuuzi huu. Iwe feki au original jifunze kuwa appreciative maana hujui ilimchukua nini kununua hiyo. Unapaswa kuwa na furaha hata yeye kakupa sababu mimi natafuta wa kunipa hata zawadi ya kitu cha bei ya chini,” mtumizi wa Instagram kwa jina Miss Chidel alikemea.

“Wakati hatimaye utakuja kubeba maji yako mwenyewe, utathamini kila tone. Natumai alijua alichoma pesa tu, haijalishi ni kidogo, alipoteza pesa hizo tu, watu kama hawa wakati mwingine hata hawajui jinsi ya kutoa, kukusanya tu bado hawawezi kuthamini,” mwingine aliandika kwa ghadhabu.

Maoni yako ni yepi?