Uzinzi unachoma sana uchumi, wanawake tu ndio hufaidika - Idris Sultan

Sultan alijizolea umaarufu ndani na nje ya taifa la Tanzania mwaka 2014 aliposhinda tuzo ya Big Brother Africa Hotshots.

Muhtasari

• “Blaza umepigwa hela ya nauli au nini?” mtumizi kwa jina Margin Call alimtania.

Mwigizaji Idris Sultan
Mwigizaji Idris Sultan
Image: Facebook

Mwigizaji maarufu nchini Tanzania Idris Sultan ameibuka na mapya ambayo yamemkuta akigombana mitandoni si tu na wanawake lakini pia na wanaume.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Sultan ambaye kando na kuwa mwigizaji pia ni mtangazaji wa redio aliibua madai kwamba uzinzi unachoma sana uchumi katika taifa lolote.

Katika kauli hiyo wengi walikubaliana naye ila sasa maoni kinzani ya kukandia yalikuja pale alipoendeleza kwa kusema kwamba wanawake tu ndio hufaidika kutokana na uzinzi na wala si wanaume.

Uzinzi unachoma sana uchumi, ni wanawake tu ndo angalau wanafanikiwa na uzinzi,” Idris Sultan aliandika.

Baadhi ya watumizi wa mtandao huo wa Twitter walimzukia na maneno mengi huku wengine wakimtania kwamab kauli hizo zake ni kama amerubuniwa nauli na mwanadada ambaye baadae hakutokea na ndio chanzo cha falsafa kama hizo kwamba wanawake tu ndio hufaidika angalau kutokana na uzinzi.

“Blaza umepigwa hela ya nauli au nini?” mtumizi kwa jina Margin Call alimtania.

“Umepiga kwnye kovu la kidonda kilichoanza kupona” Chafu Tatu aliongezea.

“Hii akili sasa hivi huwa unaitoa wapi maana ni nadra sana kusikia neno lenye afya kutoka kwako!” mwingine kwa jina Mkuu wa Kaya alimsuta.

Ila licha na masimango, wengi walionekana kuweka chuki kando na kukubalia kwa kauli hiyo yake mpaka kunukuu maandiko matakatifu kwenye Biblia yanayokemea uzinzi.

“Sio uchumi tu unamfanya anayezini awe mpumbavu kwetu sisi wakristo biblia inatuambia "azinie na mwanamke hana akili kabisa afanya jambo litakalo angamiza nafsi yake, atapata jeraha na kuvunjiwa heshima, wala fedheha yake haitafutika"Mithali 6:32,33,” mlokole huyu kwa jina Frankie alitema pointi.

Sultan alijizolea umaarufu ndani na nje ya taifa la Tanzania mwaka 2014 aliposhinda tuzo ya Big Brother Africa Hotshots. Ni mwandaji wa kipindi cha kuchekesha kwa jina Sina Habari kando pia na kuwa mtangazaji wa kituo cha redio.