Nilisaliti mke wangu kimapenzi sababu nilitaka apunguze kunona - Mwanaume aeleza (+video)

Mwanaume huyo alisema mkewe alikuwa ananona kwa kuwa na amani ya akili ndio maana akaamua kuichokora kidogo ili apunguze kunona

Muhtasari

• Alisema kwamba hilo suluhu lilifanya kazi kwani mkewe alikuwa amerudi katika mshepu wake wa kupendeza.

Unaambiwa kila mtu anayechepuka au kumsaliti kimapenzi mpenziwe ana sababu.

Mwanaume mmoja ameelezea sababu ya ajabu sana kwa mchungaji wa kanisa lake, chanzo cha kumsaliti mkewe wa ndoa ambayo mchungaji huyo aliifungisha.

Mwanaume huyo katika moja ya klipu iliyopakiwa TikTok anaeleza mchungaji kwamba aliamua kuchepuka ili kumfanya mkewe akonde.

Kulingana na mwanaume huyo, wakati alimuoa mkewe alikuwa na mshepu mzuri ila baada ya miaka michache mkewe akaongezea uzito wa mwili kitu kilichonfanya mumewe kuona kama muonekano wake haumfurahishi.

Ila kabla ya kufikia wazo la kumsaliti, mwanzo alimtuma aende gym ili kufanya mazoezi na kurudisha shepu yake ya zamani lakini bado haikufua dafu ndipo aliamua kwamba ikiwa anataka mkewe kupunguza uzito basi suluhisho ni kuhanya nje ya ndoa na kuhakikisha mkewe anajua ili apatwe na msongo wa mawazo na kupunguza uzito.

“Wakati nilimuoa mwaka 2017 kama unakumbuka mchungaji na tukafunga harusi, mke wangu alikuwa mwembamba wa kupendeza, ilipofika 2020, alikuwa ashakuwa bonge na hilo lilinitatiza sana kwa sababu nampenda mke wangu. Kwa hiyo niliamua kumtuma gym lakini bado haikusaidia,” Mwanaume huyo alieleza.

Alizidi kusema kwamab kabla ya kuchepuka alimuuliza mkewe mbona anazidi kunenepa na kuwa na shepu mbaya na mkewe akamjibu kwamba ni kwa sababu ana amani ya nafsi.

“Nilimuuliza mbona unakuwa mkubwa hivi ndio akaniambia kwamba ni sababu ana amani ya nafsi na akili. Mimi nikawaza njia pekee ya kumrudisha katika hali yake ya awali ni kuchokora amani yake ya akili na ndio nikaamua kumsaliti kimapenzi,” alieleza.

Alisema kwamba hilo suluhu lilifanya kazi kwani mkewe alikuwa amerudi katika mshepu wake wa kupendeza.

Alijitetea vikali mbele ya mchungaji wake kwamba yeye si mtu wa kudhulumu haki za mkewe kwani hata siku moja hajawahi kumchapa wala kumfanyia kitu kibaya cha kumuuliza ila tu alifanya kumsaliti ili kumpunguza unene.