Mchungaji amkaba shingoni mwanamke kanisani (+video)

Mchungaji huyo alisema alimkaba mwanamke kwa vile alihisi anaelekea kuthuru familia yake

Muhtasari

 
• “Fikiria kuwa mtu mzima na mtu anayeitwa mtu wa Mungu, lakini huwezi kudhibiti hisia zako,” Shalom Blac aliandika.

Mchungaji mmoja kutoka nchini Marekani amejipata katika gumzo chafu mitandaoni baada klipu kumuonesha akijaribu kumkaba mwakamke aliyepita mbele yake wakati wa mahubiri.

Katika moja ya video hizo zilizosambazwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii wikendi iliyopita, mchungaji huyo aliyetambulika kwa jina Lamor Whitehead alionekana akimshika shingo kwa nguvu mwanamke huyo na kujaribu kumsukuma, katika kile wengi walisema alikuwa anataka kumpiga.

Baada ya watu kuteta vikali dhidi ya kitndo cha mtumishi huyo wa Mungu, hatimaye Whitehead alinywea na kuamua kutoa tamko kuhusu kile ilichokuwa kikiwasha mihemko ya hasira mitandaoni.

Mchungaji Whitehead alisema alimzuia mwanamke huyo kwa sababu alihisi alikuwa anelekea kwenye upande amabo familia yake ilikuwa imeketi na pengine nia yake haikuwa nzuri kwa familia yake ndio maana akafanya hima kumkaba.

Ukurasa mmoja uliopakia video hiyo Instagram uliripoti kwamba mchungaji huyo alisema mwanamke huyo ni mmoja wa watu waliotumwa kusambaratisha ibada yake kanisani.

Walisema wawili hao waliletana juu mpaka kupelekea mwanamke huyo kulazimishwa kuondoka na haikujulikana nia yake ilikuwa gani na alikuwa anaelekea upande gani katika kanisa hilo pana.

“Mambo yalionekana kuzidi moto kati ya Lamor na mwanamke huyo kabla ya Lamor kuonekana akimshika shingoni na kumsindikiza nje,” The Shade Room waliripoti kwenye Instagram.

Watu wengi baada ya kuona klipu hiyo walitolea maoni tofauti huku wengine wakisema mchungaji alifanya hatua maridhawa ya kumzuia kwani angefanya kitu kibaya kwa mkewe na watoto wake. Wengine walimsuta kwamba mtu wa Mungu anafaa kuwa mfano katika kuzuia hasira zake dhidi ya watu wasiowajua.

“Fikiria kuwa mtu mzima na mtu anayeitwa mtu wa Mungu, lakini huwezi kudhibiti hisia zako,” Shalom Blac aliandika.