Wanawake maarufu walioolewa na wanaume wanaowashinda umri mara dufu

Hili gumzo liliibuka baada ya mwinjilisti Ruth Matete kusema anataka kuolewa na mzee.

Muhtasari

• Jana Matete alisema angependa kuchubiwa na mtu mzee na kuwataka vijana kukaa kando kiasi.

• Hawa ni baadhi ya wasanii na watu mashuhuri wenzake ambao wamewahi kuwa katika mapenzi na watu wakubwa kiumri mara dufu kuwaliko

Image: Maktaba

Jana mitandao ya kijamii ilipasuka kwa gumzo lenye mitazamo kinzani baada ya mwanamuziki wa injili Ruth Matete kutangaza kwamba likizo yake ya miaka miwili nje ya ulingo wa mapenzi imekamilika.

Matete alitangaza kwamba sasa yupo tayari tena kutia guu kwenye safu ya mapenzi ila kilichozua mjadala ni sharti lake kwamab ni lazima mtu atakayemchumbia kuwa mzee, kwa maana kwamba lazima mwanaume awe mkuwa kiumri kumliko.

Lakini je, kwa nini hili linazua mjadala hali ya kuwa yeye si wa kwanza kujitosa kwenye mapenzi na mtu mzee?

Hawa ni baadhi ya wasanii na watu mashuhuri wenzake ambao wamewahi kuwa katika mapenzi na watu wakubwa kiumri mara dufu kuwaliko na halikuwa gumzo, Makala haya yanalenga kuwakumbusha wale wanaomhukumu Matete kwamba yeye si wa kwanza kutokea kutaka kujaribu mahusiano na mtu mzee.

Emmy Kosgei

Msanii huyo wa injili aliyefahamika na wengi kwa vibao vya injili kwa lugha ya Kalenjin, alifunga ndoa na tajiri mkubwa Apostle Anselm Mudubuko kutokea Nigeria mwaka 2013.

 Mchungaji Anselm ni mzee kidogo kuliko Emmy, lakini hiyo haijalishi kwao sana, lakini ni muhimu sana kwa mashabiki wa Kenya, hata hivyo bado wana ndoa yenye furaha.

Wawili hao wameachana kwa pengo la miaka 20.

Mary Kilobi

Ni mwanahabari mchanga katika runinga ya KTN News ambaye ameolewa na katibu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli.

Atwoli alithibitisha kuwa ameoa Mary Kilibo, ambaye aliolewa na kuwa mke wake wa pili.

Atwoli aliongeza kuwa alihakikisha mtangazaji huyo wa Habari za Kiswahili hajaolewa kabla ya kumuoa, pia alikanusha madai ya kumpokonya msichana huyo kutoka kwa mwanasiasa mashuhuri wa Bungoma.

Inaaminika kwamba Kilobi ana umri wa chini ya miaka 40 huku mumewe Atwoli akiwa na miaka zaidi ya 70.

Betty Bayo

Ni msanii maarufu ambaye nyimbo zake zinamtukuza Mungu kwa lugha ya Kikuyu.

Bayo alikuwa katika mapenzi kwa muda mrefu na mchungaji mwenye utata Kanyari ambaye alikuwa amemuacha kiumri kwa miaka kiasi.

Walibaki pamoja kwa amani hadi kasisi Kanyari alipozuiwa baada ya kushukiwa kuwa kulaghai Wakristo wasioamini.

Baada ya kuachana, Bayo aliamua kusonga mbele na maisha ambapo mwaka jana pia alifanya ndoa ya kiasili na mchumba wake mpya.

 Bayo anaaminika kuwa na miaka 35 huku mchungaji huyo mwenye utata Victor Kanyari akiaminika kuwa na umri mkubwa kumliko.