Bahati afunguka ukimya wa mkewe Diana Marua mitandaoni

Wiki jana Diana Marua alipakia ujumbe wenye utata katika Instagram yake na kupotea mpaka leo hakuna anayejua kiini cha ujumbe ule.

Muhtasari

• Diana Marua pia ameweza kupotea mtandaoni kwa siku kadhaa sasa bila taarifa yoyote kwa wafuasi wake.

• Bahati ameongea machache kuhusu mkewe na kusema Diana hayuko kwenye hali nzuri kabisa 

Image: INSTAGRAM// BAHATI

Mwanamuziki Kevin Kioko alimaarufu Bahati Alhamis alizungumzia kupotea kwake mtandaoni baada ya kukosa kupata kiti alichokuwa akiwania cha Mathare.

Pia, ameongelea kupotea kwa mkewe Diana Marua aliyekuwa mtandaoni bado hata baada ya Bahati kupotea mtandaoni.

Kama mkewe, Bahati hajakuwa mtandaoni wala kugusia kunyamaza kwake wakati huu wote kutoka uchaguzi mkuu uliofanywa.

Hata hivyo aliweza kuonekana mtandaoni kupitia akaunti ya mkewe ya Instagram katika sherehe ya mwanao Majesty Bahati.

Diana Marua pia ameweza kupotea mtandaoni kwa siku kadhaa sasa bila taarifa yoyote kwa wafuasi wake.

Hii ni baada ya wafuasi wake wa YouTube kumfanyia sherehe ya kufana ya kusherehekea uja uzito wake na mtoto mtarajiwa.

Mama huyo wa watoto wawili na wa tatu mtarajiwa hakuwa ametaarifiwa kuhusu sherehe hiyo ndiposa akapatwa na mshangao na machozi ya furaha kumtiririka.

Sherehe hiyo iliyopangwa na wafuasi wake ilikuwa na madhari ya rangi nyeupe.

Alipotoka mtandaoni, Diana aliweka picha iliyo na giza na njiwa kisha akaandika maneno machache na kutoweka mtandaoni.

“Ni kwa giza tu ndipo unapoweza kuona nyota,”alisema.

Baada ya kuiweka picha hiyo Diana alifungia maoni juu ya chapisho hilo .

Bahati ameongea machache kuhusu mkewe na kusema Diana hayuko kwenye hali nzuri kabisa ili kudhibitisha kutoweka kwa mkewe bila ilani  mtandaoni hakuna maana fiche.

Alisema pia, yeye na familia yake hawako tayari kueleza kinachondelea kwenye familia hiyo na hata baadaye hawatazungumzia kilichojiri.

Mwanamuziki huyo aliongeza na kusema huko mbeleni, muda unapooendelea kutoweka na siku zinavyoenda yeye na Diana wataamua kama wataweza kuwaelezea wafuasi wao kisa cha kunyamaza kwake Diana.

Hata hivyo, kabla ya kupotea kwake mtandaoni Diana alikuwa amesema yeye huwa na mapambano ya uja uzito anapoelekea siku zake za tamati.

Alisema kuwa akiwa kwenye hali hiyo hana budi ila kutulia ndani ya nyumba ili kuzuia kujikaza kwingi.

"Hua nina masuala ninapokaribia kujifungua hua inafika mahali ambapo niko kwenye hali ambayo siwezi tembea, hata nikiwa kitandani mume wangu hunisaidia kugeuka. Ila kwa sasa niko sawa. Ninahangaika na mimba katika suala la kuzimia, kunenepa. Inanivunja moyo kwa sababu sikuwa tayari kupitia chanamoto hizo mara nyingine tena,” alisimulia.

Lakini alidokeza kwamba ujauzito huu umekuwa tofauti kidogo kwake kwa heri hata kama safari yenyewe imekuwa yenye changamoto si haba.