(+video) Mkono wa Bwana: Mfanyikazi wa nyumbani afurahia kupata mimba ya bosi wake

Bosi wake alianza kumtolea macho miezi miwili tu baada ya kumpa kazi na baadae akapata mimba yake.

Muhtasari

• "Nilifanya uamuzi mbaya, nikaanza kazi ya kusafisha katika nyumba hii hiyo. Miezi 2 ya kazi, alianza kunitamani kimapenzi" - Sauce aliandika.

Mwanamke mmoja aliyekuwa kijakazi wa ndani amewashangaza wanamitandao baada ya kupakia video akionesha ujauzito wake kwa furaha.

Katika video hiyo, mwanamke huyo alieleza kwamba alikuwa mfanyikazi wa ndani katika nyumba hiyo ambapo bosi wake kapera alimtongoza na kumpa mimba, tukio ambalo liimfanya kupandishwa cheo kutoka kijakazi hadi mama mwenye nyumba.

Kulingana na mwanamke huyo kwa jina Simple Sauce kwenye mtandao wa TikTok, baada ya kumaliza shule ya sekondari alibaki katika njia panda, kuchagua kati ya kufanya uchuuzi wa mwili wake kwa wanaume au kuwa mtu wa kutakatishia watu mazingira.

Alisema kwamab alilazimika kufanya maamuzi magumu na kuanza safari ambayo hakukadiria kabisa kama ingekuwa ya matumaini kwake na yenye kufungulia mirija ya baraka maishani mwake.

Alifanya uamuzi wa kuwa kijakazi kwa bosi mmoja wa kiume ambaye hakuwa ameoa.

 Katika video hiyo ambayo amepakia akicheza huku kitumbo kikionekana kabisha kuashiria dalili za kijacho, alisema baada ya kufanya kazi za ndani kwa bosi huyo kwa miezi miwili, mwajiri wake alianza kumvizia na kumtolea macho ya kumtamani kimapenzi.

Filamu ikaanza!

Kama ilivyo kawaida ya kina dada, Sauce anaeleza kuwa hakukurupuka na kukubali tu kwa vile alikuwa na dhana kwamba ni tabia ya wanaume wengine tu wanaowachezea watoto wa watu na kuwabwaga mwisho wa siku.

Baada ya tathmini ya muda, aliamua kufanya jaribio la kumpa nafasi na katika mchakato wa kula uroda, matokeo yake yakawa ni mimba. Mimba ambayo ilimpa nafasi ya kupandishwa cheo kuwa mama mwenye nyumba kutoka kwa kijakazi.

“Kutoka kwa msafishaji wa kawaida hadi mama wa nyumba. Baada ya shule ya upili, nilikuwa na maamuzi mawili. Kufanya udangaji au upate kazi nzuri. Nilifanya uamuzi mbaya, nikaanza kazi ya kusafisha katika nyumba hii hiyo. Miezi 2 ya kazi, alianza kunitamani kimapenzi. Nilidhani ni mwanaume kuwa mwanaume. Sikujua ni mkono wa Mungu juu ya maisha yangu,” Simple Sauce aliandika kwenye video hiyo kwa furaha na tabasamu ghaya.