• Mwanaume huyo alisema ombi hilo la kutaka maam mkwe kuondoka lilipata upinzani mkali kutoka kwa mkewe ikabidi akawafukuza wote.
• "Usiku uliisha mke wangu akiwa amelala nyumbani kwa wazazi wake,” bwana harusi alieleza.
Mwanaume mmoja amewashangaza wanamitandao baada ya kuelezea matukio yaliyotokea katika harusi yake mpaka kusababisha yeye kumfurusha mama mkwe wake.
Kupitia mtandao wa Reedit, mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina Senior Koala, alielezea kwamba marashi ya maam mkwe yalimchefua vibaya mpaka ikamlazimu kuchukua uamuzi wa kumfurusha kabisa, ambapo pia mke wake alijaribu kuteta wakaongozana na mamake.
Mwanaume huyo alielezea kwamba katika mara kadhaa ambapo alikuwa anakutana na mama mkwe kabla ya harusi, mama mkwe hakuwa mtu wa kutumia marashi na walikuwa wanazungumza vizuri.
Lakini siku ya harusi bibi harusi mtarajiwa alimteua mamake kuwa mmoja wa wasimamizi wa shughuli zote na walikuwa jukwaani katika sehemu bana ambapo alimkaribia mama mkwe na harufu ya marashi yake ikamchefua.
“Mke wangu alichagua na mama yake kuwa matron wake wa heshima kwa hivyo alikuwa amesimama nasi mbele. Lilikuwa eneo dogo na nikiwa naye karibu kabisa na mke wangu, niliweza kunusa manukato yake. Muda mfupi baada ya sherehe kuanza nilianza kutokwa na machozi na kunusa. Sherehe yetu ilitakiwa kudumu kwa dakika 20 tu kwa hivyo nilidhani ningesukuma isipokuwa iwe mbaya zaidi,” Koala alieleza.
Sakata zima lilianza pale walipomaliza harusi na kuelekea sehemu ya mapokezi ambapo ilikuwa lazima kuchukua picha za pamoja na wanafamilia. Yeye alishindwa kabisa kustahimili harufu ya marashi ya maam mkwe na ndio alimtaka mkewe kulizungumzia.
“Nilimwambia mke wangu tunahitaji kujua kitu kwa sababu dalili zangu hazikuwa zikipungua na sikutaka kujiondoa katika kuchukua dawa zaidi kwa ajili ya mapokezi yetu au kuondoka mapokezi yetu wenyewe. Mke wangu alimwomba mama yake kuweka umbali kati yetu ili kujaribu kunirahisishia. Haikufua dafu,” mwanaume huyo alieleza.
Baada ya watu kutoa suluhu zote ambazo hazikuonekana kufua dafu, mwanaume huyo bwana harusi aliamua liwalo na liwe, aligonga msumari juu ya kichwa kwa nyundo!
“Nikasema kuna jambo lingine nikapendekeza labda mama mkwe aondoke akabadili nguo kisha arudi au hata aende tu kwenye duka la kuuza vitu jirani na kununua nguo za aina yoyote, hata ningelipia. Nilimuomba mama mkwe wangu aidha afanye hivyo au aondoke tuje tutembelee baadae na keki maana ilifikia hatua ya kunihitaji kuondoka,” alisema.
Hili lilipingwa vikali na mama mkwe pamoja na bi harusi, ukawa mlima mkubwa wa kuupanda kwa bwana harusi. Ikabidi atumie busara ya mfalme Suleiman kung’amua mambo.
“Naelewa siku ilikuwa kubwa kwa mke wangu na alimtaka mama yake pale na mimi nilimtaka huko pia lakini sikuweza kufurahia harusi yangu mwenyewe. Usiku uliisha mke wangu akiwa amelala nyumbani kwa wazazi wake,” bwana harusi alieleza.