Dada, Kama hujachumbiana na mwanaume Mjaluo bado uko singo - DJ Pierra Makena

Ushauri huo wa mama wa mtoto mmoja ulikuwa umewalenga wanawake wote, iwe umeolewa au bado

Muhtasari

• Matamshi haya yaliibua mjadala mkali kwenye post hiyo huku wengine wakisema kwamba huenda mama huyo wa mtoto mmoja ameangukia penzi la Mjaluo.

Mcheza santuri Pierra Makena anatoa ushauri kuhusu kuchumbiana
Mcheza santuri Pierra Makena anatoa ushauri kuhusu kuchumbiana
Image: instagram

Mcheza santuri wa muda mrefu ambaye aliinua jina la kike katika Sanaa hiyo iliyokuwa inatawaliwa sana na wanaume, Pierra Makena ameibua jipya kuhusu kuchumbiana.

Kupitia Instagram yake, Makena ambaye ni mama wa mtoto mmoja alishangaza wengi ambapo alisema kwamba mwanamke yeyote iwe ameolewa au hajawahi kuolewa, kama hajawahi kuchumbiana na mwanaume kutoka jamii ya Waluo basi huyo ni singo rasmi.

“Mwanamke ambaye hajawahi kuchumbiana na mwanaume kutoka jamii ya Wajaluo bado yupo singo. Nani mwingine ana maoni?” Pierra Makena aliandika.

Matamshi haya yaliibua mjadala mkali kwenye post hiyo huku wengine wakisema kwamba huenda mama huyo wa mtoto mmoja ameangukia penzi la Mjaluo.

Wengine walipinga kauli hiyo kwa kusema kwamba wanaume kutoka jamii huyo wana hulka za kuonesha mapenzi kwa mabinti sana ila pia ndio wana mazoea ya kuvunja roho za mabinti wengi baada ya kuzama katika penzi lao.

“Nadhani inafaa kuwa kama Mwanamke ambaye hajachumbiana na mwanamume wa Kijaluo bado yuko katika madarasa ya awali ya kuvunjwa kwa roho,” mwingine kwa jina George Githuma aliandika.

Itakumbukwa Makena ana asili kutoka jamii ya Ameru na kupakia kwake kwa maneno hayo kulifanya wengi kushindwa kuelewa kama kauli hiyo inamaanisha kuwa mtu kama hajachumbiana nao bado hajajua mapenzi au la.

Na si Wameru mnapenda kusema ukweli Lol…lakini kuwa tu tayari kuwa mmoja wa wapenzi kwa sababu watu hawa wanaamini sana katika kushirikiana kama njia moja ya kujaliana,” mwingine alimtahadharisha.