"Mimi kuingia kwenye uhusiano inawauma watu aje" - Willy Paul awasuta wanaomsema

Willy Paul aliwasuta watu baada ya madai ya kuwa anamtaka mpenzi wa wenyewe.

Muhtasari

• Jamaa mmoja ameibuka akisema kwamba msanii Willy Paul anamvizia na kumtolea macho ya mapenzi mpenzi wake.

• Jamaa huyu alidai sababu ya kusema hivyo ni kuwa Willy Paul alikuwa kwenye inbox ya mpenzi wake na amekuwa akishinda akimtumia ujumbe kwenye Instagram na Tiktok.

Willy Paul na Jovial wadokeza kuwa kwenye mapenzi
Willy Paul na Jovial wadokeza kuwa kwenye mapenzi
Image: Instagram

Mwanamuziki Wilson Abubakar Radido alimaarufu Willy Paul awasuta watu baada ya madai ya kuwa anamtaka mpenzi wa wenyewe.

Mtu huyo alituma ujumbe wa siri kwa blogu moja ya humu nchini akiambatanisha na picha za kudhibitisha madai kuwa Pozee alikuwa anataka mpenzi wake.

Jamaa huyo alidokeza kuwa hata baada ya Pozee kuweka wazi kuwa huenda yeye na msanii wa kike Jovial wako katika mahusiano bado hajatosheka naye na anataka kujilimbikizia mpenzi mwingine kutoka kwa jamaa huyo.

Jamaa huyu alidai sababu ya kusema hivyo ni kuwa Willy Paul alikuwa kwenye DM ya mpenzi wake na amekuwa akishinda kumtumia jumbe mpenzi huyo wake kwenye Instagram na Tiktok.

Aliweza kutuma picha iliyoonyesha Willy Paul kutaka kuwa rafiki ya mpenzi wa jamaa huyu kwenye mtandao wa TikTok.

Image: Nairobi Gossip
Image: Nairobi Gossip
Image: Nairobi Gossip

"Nilijua tu huyu lazima angenitumia ujumbe kwenye DM, na Jovial ako tu mahali hana wasiwasi na huyu," alisema dada huyo.

Willy Paul aliweza kujibu ujumbe huo ulioanikwa kwenye mtandao na Nairobi Gossip na kusema yeye alishapata mchumba wake na ametosheka na huyo.

Aliwakejeli watu ya kuwa wanamwonea wivu na wanahsisi uchungu kuwa amepata mpenzi na ako kwenye uhusiano wa dhati sasa.

"Haha kwani mimi kuwa kwenye uhusiano imeumaje watu. Endeleeni, mimi nishapata wangu," alisema.

Aliongeza pia ya kuwa uhusiano wake na Jovial hauwezi ukavunjwa na mtu yeyote kwani dhamana iliyomo baina yake na mpenzi wake si hivi hivi na kuwa washachelewa wale wa kamati ya roho chafu.

Watu waliweza kumkejeli jamaa huyo kuwa anataka kutumia jina la mwanamuziki huyo ili kutafuta kiki.

Baadhi ya maoni ya watu ni:

@its_keitany-Sasa huyu anajivunia ati "huskii Pozee anamtaka mamaa".

@ciciuna_jnr-@willy.paul.msafi waambie Willy, hawa watu hawatawahi elewa . Si kila kitu inahusu mahusiano haswa mtu akikutumia ujumbe. Wengine wenu sijui mna fikra zipi.

@eugleene-Wanaume wenzake huku nje anatafuta pesa huyu anafuatilia mtu anamtumia mpeni wake ujumbe.

Uhusiano wa Jovial na Willy Paul bado unaonekana kuwa kiki na mashabiki wao.