Mwanasoshalaiti Vera Sidika afichua kilichoongeza ukubwa wa makalio yake

Mwanasoshalaiti huyo alikiri kuwa ukubwa wa makalio yake ulikuwa ukimfanya awe na aibu sana.

Muhtasari

•Mama huyo wa binti mmoja sasa ameweka wazi kuwa makalio yake asili na hakuwahi kufanyiwa upasuaji wa kuyafanya makubwa zaidi.

•Vera hata hivyo ameshikilia kuwa matiti yake sio asili na kuweka wazi kuwa alifanyiwa upasuaji ili kuongeza ukubwa wake.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti maarufu Vera Sidika amekuwa gumzo kote mitandaoni kwa siku kadhaa sasa. Amekuwa akivuma tangu mapema wiki jana wakati ambapo aliibua madai kuwa alifanyiwa upasuaji wa kuyapunguza makalio yake, madai ambayo aliyazika baadaye alipoachia ngoma na ikabainika kuwa yote yalikuwa kiki tu.

Mama huyo wa binti mmoja sasa ameweka wazi kuwa makalio yake asili na hakuwahi kufanyiwa upasuaji wa kuyafanya makubwa zaidi.

Jumatatu, akiwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram, mwanasoshalaiti huyo hata hivyo alidokeza kuwa dawa za kupanga uzazi alizokuwa akitumia zilichangia ukubwa wa makalio yake.

"Je, makalia yako ni asili? Kuwa mwaminifu?" mtumizi mmoja wa Instagram alimuuliza mwanasoshalaiti huyo.

Katika jibu lake, alifichua kuwa awali kabla hajahamia jijini, ukubwa wa makalio yake ulikuwa ukimfanya awe na aibu sana.

 "Ndiyo. Siku zote nimekuwa na makalio ma ubwa na siku zote nilikuwa nikiaibika hadi nilipofika Nairobi ambapo kila mtu alinifanya nihisi kama ni ya thamani sana.. Jambo ni kwamba, niliongeza uzito kwa sababu ya kupanga uzazi na hivyo makalio yaliongeza uzito pia." alisema.

Alifichua kuwa alipokuwa katika shule ya upili alikuwa amebandikwa jina 'Wezere' (Makalio) kutokana na ukubwa wake.

Katika kipindi hicho, pia alikiri kuwa umaarufu wake ulianza kupanda baada ya kushirikishwa kwenye video wa wimbo 'You Guy'  wa P-Unit takriban mwongo mmoja uliopita. Baada ya kuonekana kwenye video ya wimbo huo, Wakenya wengi walibaki wakizungumzia saizi ya makalio yake na kufuatia hayo akaalikwa katika vyumba mbalimbali vya habari kwa ajili ya mahojiano.

Vera hata hivyo ameshikilia kuwa matiti yake sio asili na kuweka wazi kuwa alifanyiwa upasuaji ili kuongeza ukubwa wake.

"Ilinigharimu dola 20,000(2.4M)" alisema.

Wiki iliyopita mwanasoshalaiti huyo alikuwa ameteka mitandao ya kijamii baada ya kupakia picha iliyofanyiwa ukarabati ambayo ilionyesha akiwa na makalio makubwa. Alidai kuwa alilazimika kufanyiwa upasuaji kutokana na sababu za kiafya.

"Wanadada tafadhalini, mjue kujipenda mlivyo na msikubali shinikizo la rika liwafanye mkimbilie kufanya mambo ambayo yatawaharibia maisha yenu huko mbeleni. Nina bahati kuwa hai. Sikusherehekea siku yangu ya kuzaliwa mwaka huu, lakini tuko hapa sasa. Heri ya kuzaliwa kwangu. Nimekuja kushukuru kuwa na uhai na kutoyachukulia mambo yoyote hivihivi," alisema wiki jana.

Baadaye alijitokeza kubainisha kuwa alitumia madai hayo kutafuta kiki kwa ajili wimbo wake mpya wa kufoka  'Popstar.'