Trevor Ombija atetea kelele za klabu yake, asema walalamishi ni wachache

Alisema akiwa kwenye mkutano wa wamiliki wa baa na wakaazi wa Kileleshwa

Muhtasari

• Alisema kuwa jirani yake alikuwa anateta kuhusu kelele iliyokuwa inatoka kwenye klabu hiyo yake na alikuwa anataka ifungwe.

• Alijitetea pia na kusema kuwa migahawa isiyo ya vilevi pia ilikuwa kwenye orodha ya migahawa ambayo inafaa kufugwa licha ya kutokuwa na leseni ya mvinyo.

Katika mkutano wa wamiliki wa baa na migahawa na wakaazi wa kileleshwa, Mwanahabari Trevor Ombija ambaye pia ni mmilik iwa sehemu ya kujivinjari na baa ya Samaki Samaki amejitetea baada ya madai ya kuwa klabu hiyo huwa na kelele.

Alisema kuwa jirani yake alikuwa anateta kuhusu kelele iliyokuwa inatoka kwenye klabu hiyo yake na alikuwa anataka ifungwe.

Ombija alisema dada huyo alikuwa anasisitiza klabu hiyo ifungwe kwa kuwa alikataa kumpa kazi.

"Majirani wengine hawajalalamika na jambo hilo ila yeye tu ndiye aliyekuwa akisisitiza klabu hiyo ifungwe," Ombija alisema kwenye..

Aliongeza kuwa alijaribu kumpa dada huyo chaguo la kuweka vizuia sauti kwenye nyumba yake ili kuzuia sauti kuingia.

Ombija alifafanua kuwa mwanadada huyo alikataa na alianza kuwazuia wateja kuegesha magari yao nje ya nyumba yake.

Alijitetea pia na kusema kuwa mikahawa ya kikanisa pia ilikuwa kwenye orodha ya migahawa ambayo inafaa kufugwa licha ya kutokuwa na leseni ya mvinyo.

"Kuna madai na malamishi ya kweli ambayo yanafaa kutatuliwa ila pia kuna malalamishi ambayo si ya kweli  na yanafaa kutupiliwa mbali," Ombija alisema kwa ukurasa wake wa Twitter.

Alisema kuwa maneno ya mtu mmoja hayafai kusababisha wengine kuingia kwenye chuma moto cha kukosolewa.

MCA wa Kileleshwa Robert Alai hakufurahiswa na tukio hilo na alivyojitetea Ombija na kusema kuwa suluhisho alilopendekeza mwanahabrui huyo si la maana.

"Ukitaka kuona kichaa kwenye sekta ya burudani nchini Kenya, tizama hii.Mmiliki wa bar iliyo na kelele Kileleshwa apendekeza kuwaekea wakaazi wa huko vizuia sauti kwenye nyumba zao. Tuna watu wanaofikiria bado kweli?" mwanablogu huyo alisema.