Vera Sidika kuangazia zaidi talanta yake ya muziki

Sidika alisema kuwa mume wake Brown Mauzo alimuunga kurekodi wimbo wake

Muhtasari

• Alieleza maana ya wimbo wake mpya wa Popstar na kusema kuwa wimbo huo unaongelea maisha yake.

• Sidika alifichua kuwa alirekodi wimbo huo nyumbani kwake kwani kuja studio kwenye mandhari ya nyumba yake na kuwa hakuchukua muda mrefu.

Vera Sidika

Mwanasosholaiti nchini  Kenya Vera Sidika ameeleza kuwa anapanga kuangazia sana taalum yake ya mziki.

Sidika alisema kuwa anapenda kuimba kwa kuwa taalum hiyo haina vizuizi na anaweza kufanya jambo lolote akiwa msanii.

Alieleza maana ya wimbo wake mpya wa Popstar na kusema kuwa wimbo huo unazungumzia maisha yake.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kuwa hata watu wakitoa maoni yasiyopendeza kuhusu wimbo wake mpya hana shida nayo.

"Siwalazimishi watu kupenda muziki wangu kwa kuwa watu wana maoni tofauti na hisia tofauti za kimuziki ni jambo ambalo huwezi uka..," Sidika alisema.

Mwanasosholaiti huyo alisema kuwa mume wake, mwanamuziki Brown Mauzo amemuunga mkono sana kwenye sekta yake ya muziki.

Sidika alifichua kuwa alirekodi wimbo huo nyumbani kwake kwani kuja studio kwenye mandhari ya nyumba yake na kuwa hakuchukua muda mrefu.

Alisema wimbo wake Popstar wamzungumzia yeye katika maisha yake ya hapo awali kabla ya kuwa maarufu.  Kulingana naye amezungumzia umaarufu wake na maisha yake akiwa na pesa kwenye wimbo huo.

Alizungumzia tatizo ambalo liko kwenye mtandao wa YouTube la wimbo wake kutotokea unapotafutwa.