Saa hii mimi ni bibi ya Yesu - Vivianne amjibu shabiki aliyejaribu kumtongoza

Vivianne aliongelea hali yake ya sasa na alivyoamua kuzingatia maisha yake na Mungu

Muhtasari

• Vivianne alisema kuwa hakuwa anatarajia matukio yaliyotukia kwenye maisha yake hivi majuzi lakini hana budi ila kukubali.

vivian (1)
vivianne vivian (1)

Mwanamuziki Vivian amemjibu shabiki yake mmoja aliyejaribu kumtongoza baada ya kupakia picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Shabiki huyo alijaribu kumshawishi Vivianne awe mchumba wake akiashiria hali ambayo mwanamuzki huyo yuko kwa sasa.

Alimwomba Vivianne kumpa nafasi hiyo ya kuwa mpenzi wake ili awze kumpa furaha, hali ambayo hajakuwa nayo kwa muda sasa.

"Kwa sasa ambapo hauko kwenye mahusiano,nipe nafasi niwe mchumba wako,  nilicho nacho unakihitaji wewe," Edwinthairu alimwambia Vivianne.

Mwanamuziki huyo alimjibu Edwin kwa matani akisema kuwa yeye hayuko tayari kuwa kwenye uhusiano kwa sasa.

Alisema kuwa kwa sasa amejitosa kanisani na kuamini Mungu na huo ndio uhusiano ambao anataka.

"@edwinthairu wuui saa hii mimi ni bibi ya Yesu," Vivianne alimwambia shabiki huyo.

Edwin hakukata tamaa na aliendelea kumrushia mistari mwanamuziki huyo na kumwambia kuwa wajaribu kuwa wachumba bado.

Alisema kwamba atakuwa akiandamana na Vivianne kanisani kila Jumapili ili kuelewa uhusiano wake na Mungu.

Vivianne alikuwa amepakia picha Instagram aliyoonekana kuwa na mwonekano mpya na kuzungumzia maisha yake yalivyo sasa.

Alisema kuwa alilazimika kukubali hali yake kwani hakuwa amejitayarisha kwa kilichotendeka katika maisha yake.

"Niligundua kuwa chochote nilichofanya, kusema ama nilivyokuwa sijajiandaa kuyapokea mabadiliko katika maisha yangu, ilikuwa kadri ya uwezo wangu," Vivianne aliandika.

Aliongeza kuwa aliamua kuangazia kwa undani suala lake na Mungu ili aweze kuyasahau mawazo yake.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa bado hajapangia matukio yake ya mbeleni na ana matumaini ya kuongozwa na Mungu.