Nadia Mukami afichua sababu ya kunyoa nywele zake

Nadia ameeleza mabadiliko hayo yake ya baada ya kujifungua

Muhtasari

• Mukami hajanyoa nywele tu, bali pia majaribu kuupunga mwili wake baada ya kujifungua na kuongeza mwili.

• Mwanamuziki huyo alikuwa amesema kuwa muda baada ya kujifungua si rahisi kwake kama kuubeba uja uzito.

Nadia mukami
Image: Nadia Mukami Instagram

Mwanamuziki Nadia Mukami alieleza sababu yake ya kunyoa nywele zake na kuwa na muonekano mpya.

Mukami alinyoa nywele zake siku chache baada ya kujifungua na amekuwa akitumia nywele bandia anapoenda kwenye shoo zake.

Katika ukurasa wake wa Instagram, mwanamuziki huyo alisema kuwa alinyoa nywele zake baada ya kujifungua kwa sababu nywele zake zilianza kukatika akinyonyesha.

"Hakuna sababu nyingine iliyofanya ninyoe nywele zangu,hairline yangu ilipotea," Mukami alieleza kwenye video yake.

Alisema kuwa amekuwa akifurahia jukumu lake la ulezi ila haijakuwa rahisi kwake kwa kuwa hangekuwa na muda wake kivyake.

Mwanamuziki huyo pia alirudi kufanya mazoezi ili apunguze mwili wake ambao uliongezeka baada ya kujifungua.

Alisema kuwa alikuwa amejaribu kufanya mazoezi mtoto wake alipofikisha miezi mitatu ila ilimbidi awache ili kumshughulikia mwanawe.

"Niliacha kufanya mazoezi wakati huo kwa sababu maziwa yalikuwa yamepungua kwenye matiti yangu, ilibidi niwache ili mtoto ashibe," mama huyo wa mtoto mmoja alisema.

Aliongeza kuwa amerudi kufanya mazoezi baada ya mtoto wake kufikisha miezi sita, na amefurahia kupata wakati wa kibinafsi ili afanye mazoezi.

Mpenzi huyo wa Arrow Boy alisema kuwa sababu yake ya kutaka kufanya mazoezi ni kuwa kuna hafla nyingi atakazohudhuria.

Mukami alisema kuwa hafla hizo zinamhitaji akiwa anajiweza ili asiweze kuchoka haraka baada ya hafla moja.

"Nimerudi kufanya mazoezi, kwa sasa nina kilo 67 na ninapswa kuwa na kilo 60, ni jukumu kubwa kuwa mama na msanii kwa wakati mmoja. Naupenda mwili wangu ulivyo sasa, na makalio yalivyokuwa makubwa ila bado nafaa kupunguza mwili," Mukami alieleza sababu yake.

Takriban miezi sita iliyopita,Arrowboy na Nadia walimkaribisha mwanao Haseeb Kai duniani.