(+video) Mama ashindwa kuzuia machozi binti yake aliyefungwa jela miaka 7 akirejea nyumbani

Katika video hiyo, mama anaonekana akichungulia kutoka kwa nyumba baada ya kuona gari nje la lango lake na kumuona bintiye.

Muhtasari

• Mama huyo anaona gari liliingia kwenye ua la nyumba yake na alipotoka alikuta na bintiye aliyekwenda jela miaka 7 anashuka na kumkumbatia kwa furaha.

Mwanadada mmoja alipakia video kwenye mtandao wa TikTok akionesha jinsi alimtembelea mamake kwa kumshtukia pasi na taarifa yoyote baada ya kuhudumia kifungo cha miaka saba jela.

Mwanamke huyo, aliyetambuliwa kama @itss_kb1 kwenye TikTok, alifichua kwamba alikuwa gerezani kwa miaka saba iliyopita. Baada ya kuachiliwa, aliendesha gari hadi nyumbani kwa mama yake bila taarifa mapema kuhusu kuwasili kwake kwani alitaka liwe tukio la kushtukiza.

Baada ya kujaribu kujikusanya pamoja kutokana na mshtuko huo, mama alinyoosha mikono yake na kumkumbatia bintiye kwa nguvu, karibu kutiririkwa na machozi ya furaha.

“Baada ya miaka saba jela, hatimaye niko huru na nilimshtukizia mama yangu,” mwanadada huyo aliandika kwenye video hiyo.

Ingawa mwanadada huyo hakueleza kilichompeleka jela, tukio la video hiyo lilizua maoni kutoka kwa wanamitandao huku baadhi wakifurahia na kusifia upendo wa mama kwa mwanawe kama upendo ambao hauna mfano duniani.

“Mama alimkosa mtoto wake bila shaka ❤️Natumai mambo yanakwenda vizuri kwako leo,” mtumizi wa Tiktok kwa jina Ophelia aliandika.

“Nilihudumu kwa miaka 19 kama mlinzi mkuu wa magereza, nakumbuka sana matukio kama haya kuwaona kina baba na mama katika malango yale wakija kuwaona watoto wao wafungwa,” Xavier Green alisema.

“Kama mama ambaye mtoto wa kiume wangu amekuwa gerezani naweza kukuambia roho ya mama yako na moyo umekamilika mara tu alipokuona tukio la kushtukiza nzuri hili,” mama kwa jina Koori Queen alidokeza kuwa mmoja wa wale wanaowakosa watoto wao ambao pia wanahudumia kifungo jela.