"Baba mwenye fahari!" Kabi Wajesus ajivunia baada bintiye wa miezi 6 kutobolewa masikio

Kabi alidokeza kuwa watatambulisha wazi sura ya binti huyo wake hivi karibuni.

Muhtasari

•Kabi Wajesus alitangaza habari za kutobolewa kwa bintiye siku ya Jumatatu na kusema kuwa anajivunia hatua hiyo.

•"Yeye ni malkia wa urembo," Kabi  alisema.

Kabi na Bintiye wa Miezi sita
Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Wanandoa Peter Kabi na Millicent Wambui wa The Wajesus Family wametoboa masikio ya binti yao wa miezi sita.

Kabi Wajesus alitangaza habari za kutobolewa kwa bintiye siku ya Jumatatu na kusema kuwa anajivunia hatua hiyo.

"Mimi ni baba mwenye fahari baada ya mtoto kutobolewa.. mtoto wako alitobolewa akiwa na umri gani?" alisema kupitia Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha iliyomuonyesha akiwa amemkumbatia binti yake kwenye mikono yake. Pichani, inaonekana wazi kuwa mtoto huyo wa pili wa wanandoa wa Wajesus amekuwa mkubwa sana.

Katika sehemu ya maoni, Kabi aliwahimiza wazazi wengine kuwatoboa binti zao wangali katika umri mdogo.

"Unapaswa kujaribu, ama hutaki atoboe sasa," alimshauri mama mmoja wa binti wa miaka saba aliyetoa maoni.

Pia alidokeza kuwa atatambulisha wazi sura ya binti huyo wake hivi karibuni.

"Yeye ni malkia wa urembo,"  alisema.

Kabi na Milly Wajesus walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili pamoja mapema mwezi Aprili, mwaka huu.

Wanandoa hao walivunja habari hizo njema kwa mashabiki wao siku kadhaa baada ya binti yao kuzaliwa.Walieleza kuwa walichelewesha hatua ya kumtambulisha kwa kuwa bado walikuwa wakijiandaa kwa hali yao mpya.

"Tumekuwa na mtoto kwa siku chache. Tulihisi tulihitaji kutulia mtoto kwanza aje nyumbani tumuelewe, nikumbuke kuosha mtoto, kumshika na kumyonyesha. Imechukua muda kutulia na mtoto," Milly alisema kupitia YouTube.

Binti huyo wa nusu mwaka ni mtoto wa pili kwa Milly na wa tatu kwa Kabi ambaye aliwahi kumtambulisha binti yake mwingine, Abby Wajesus ambaye alizaliwa takriban miaka tisa iliyopita.