Baba wawili wafika shuleni kuchukua binti zao, wapata ni binti mmoja, warushiana ngumi

Baba hao walijikuta katika kupigania binti mmoja, kila baba akisema ni binti wake halali.

Muhtasari

• Kama haitoshi, wanaume hao wawili walipata kila mmoja wao ameandikishwa kama mtu wa karibu wa mtoto yule.

Vobonzo vya wanaume wawili wakinuniana
Vobonzo vya wanaume wawili wakinuniana
Image: Vecteezy

Kioja kilitokea katika shule moja nchini Marekani baada ya wanaume wawili kufika shuleni kwa ajili ya kila mmoja kumchukua binti yake nyumbani lakini wote wakashtuka kupata kwamab nib inti yule mmoja ambaye kila mwanaume alikuwa anasema ni mtoto wake.

Kulingana na jarida la Fox 28, mwanadada mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi katika shule hiyo alirekodi video kadhaa za tukio hilo na kupakia kwenye mtandao wa TikTok, tukio ambalo liligeuka kuwa kama filamu ya kuchekesha ya Mr Bean.

“Wanaume hao walikuja kabla ya watoto kufunga shule mapema mwezi huu - kila mmoja akidai msichana huyo ni binti yao na kwamba walitaka kumchukua kwa siku hiyo. Na hivyo, wote wawili walitazamana, na kila baba alikuwa kama, 'Kwa nini unamchunguza mtoto wangu? Wewe ni nani?” Fox 28 walinukuu moja ya video hizo.

Huku mwanaume mmoja akimuuliza mwenzake ni kwa nini anamwangalia binti yake, wa pili akamjibu kwamba huyo ni binti yake pia.

Kama hilo halitoshi, mwanadada huyo mwenye video alieleza kwamba wanaume hao wote wawili walikuwa wameandikishwa kama watu wa karibu na binti huyo na hata nambari zao za vitambulisho kuchukuliwa na uongozi wa shule.

Hali iligeuka kuwa kioja kikubwa wakati mamake binti huyo alipigiwa simu akitakiwa kufika shuleni hapo huku wanaume wale waliokuwa wamevimbiana karibu kukabana koo wakitenganishwa huku mama mtoto akisubiriwa kuja na suluhisho kamili kuhusu ni nani baba halali kwa binti yake.

Mama huyo alisema alikuwa akiwaambia wanaume wote wawili kuwa wao ni baba wa msichana huyo - ambaye hakuwepo kwa madai ya tukio hilo.

“Hakuna aliyewahi kujua chochote.... Huu ulikuwa wazimu. Lakini, mwisho wa siku, polisi walikuwa pale. Mmoja wa akina baba alifungwa. Unajua, mama alienda kwa EMS. Nyanya alilazimika kuja kumchukua mtoto, kwa sababu hakuna mtu ambaye angeweza kukabidhiwa mtoto wakati huo," Fox 28 waliripoti.