Harmonize amshukuru Kajala kwa kuchangia pakubwa katika albamu yake mpya

Mwanamuziki huyo alitangaza kufichua albamu hiyo mnamo Oktoba 28

Muhtasari

• Harmonize alimwandikia Kajala ujumbe wa shukran kwa kazi aliyofanya na kumfikisha alipo sasa ambapo amekamilisha albamu hiyo.

•Harmonize aliwashukuru wengine waliomsaidia kukamilisha albamu yake;

Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Staa wa Bongo Harmonize ametoa shukran za dhati kwa mchumba wake Frida Kajala Masanja kwa kumsaidia katika albamu yake mpya ya Made For Us.

Kwenye Instagram, Harmonize alimwandikia Kajala ujumbe wa shukran kwa kazi aliyofanya na kumfikisha alipo sasa ambapo amekamilisha albamu hiyo.

"Umeifanya akili yangu iwe na utulivu, naweza tunga mistari inayostahili. Ulifanya kazi kubwa zaidi kuboresha albamu hii. Asante na nakupenda, mke wangu na boss wangu," Harmonize alimwambia Kajala.

Kajala pia alimpongeza mpenzi wake kwa hatua hiyo kubwa baada ya mwanamuziki huyo kutangaza kuwa atafichua albamu hiyo mnamo Oktoba 28.

Alisema kuwa nyimbo hizo za albamu yake zilirekodiwa kwenye studio na kuwa hakutaka kuzifanyia kiki.

"Chapisho moja labda,nimewarekodia watu wangu wa Afrika Mashariki na kila mtu anayezungumza lugha ya Kiswahili duniani. Oktoba 28 ni siku ya kusherehekea," Harmonize aliwafahamisha mashabiki wake.

Harmonize aliwashukuru wengine waliomsaidia kukamilisha albamu yake;

"Kakangu Zungu bboybeats, nina deni kubwa sana kwako. Asante kwa kuifanya sauti yangu iwe nzuri zaidi ya kuskika. Ulichofanyia albamu hii, Mungu akubariki," Harmonize alimshukuru.

"Asante Boss wangu mkubwa @choppa_tz, mimi humpa muziki kijana huyu kabla ya mipango yoyote ile. Big Love Baba," mwanamuziki huyo alimwandikia @erikasaragoni.

"Kakangu mkubwa, nakupenda. Mneki umekuwa kiongozi mwenye busara unanitahisishia mengi sana, ulifanya kazi nzuri kwa albamu hii inayofuata," Harmonize alimwambia @jembenijembe.