Mapenzi sumu, jamaa abomoa nyumba alizojengea mama mkwe

Mwanamke alimtumia ujumbe kumjulisha kwamba amempa talaka licha ya kuwa na watoto watatu naye.

Muhtasari

• Mke wa Banda alimuacha na kwenda kwa mwanaume mwingine, jambo ambalo lilimuuma sana.

Mwanamume mmoja mchini Malawi aligonga vichwa vya habari baada ya kubomoa nyumba mbili alizokuwa amejengea mama mkwe kwa hasira baada ya  kuachwa na mkewe.

Francis Banda aliomba usaidizi kwa marafiki wake ili wamsaidie kubomoa nyumba hizo mbili alizokuwa amejengea mkewe na mama mkwe.

Mke wa Banda alimuacha na kwenda kwa mwanaume mwingine, jambo ambalo lilimuuma sana.

Mwanamke alimtumia ujumbe kumjulisha kwamba amempa talaka licha ya kuwa na  watoto watatu wa jamaa huyo.

Banda alifichua kwamba wakati wa ndoa yao, alijituma sana kuwajengea wazazi wa mke wake nyumba ya kifahari ili waishi maisha ya starehe kijijini.

 Licha ya hilo mke wa Banda aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine na kuhamia kwa bwanake mpya.

Mke wa Banda alisaliti ndoa yao ya miaka 13.

"Wakati mwingine jamani, nilijaribu kuwasiliana na mke wangu lakini simu yake ilipokelewa na mpenzi huyo mpya," Banda alisema.

Video hiyo iliyopakiwa kwenye mtandao wa Instagram ilifanya watu kutoa hisia kinzani huku wengi wakisema jamaa huyo hakufanya jambo la busara kubomoa nyumba hizo.

''Tunaelezea hasira yetu kwa njia tofauti, lakini hii imezidi. Nini kingetokea kama angeuza nyumba?'' feezah.08 aliuliza.