Aliyejifanya mwanamke ili kupata kazi ya 'maid' akamatwa kwa kumlawiti mpwa wa bosi

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa amefanya kazi kama mjakazi kwa miezi mitano pasi na kugundulika kuwa ni wa jinsia ya kiume.

Muhtasari

• Mukutindwa alijaribu kulawiti mpwa wa tajiri wake kalba ya kuzidiwa nguvu na kijana huyo ambaye alimripoti na kukamatwa.

Mukutindwa, mtuhumiwa wa ulawiti aliyejifanya mwanamke
Mukutindwa, mtuhumiwa wa ulawiti aliyejifanya mwanamke
Image: Facebook

Mwanaume mmoja aliyejifanya kuwa mwanamke ili kupata kazi ya ndani kama kijakazi amekamatwa baada ya kujaribu kumlawiti mpwa wa tajiri wake.

Mwanaume huyo aliyetambuliwa kama Christoher Mukutindwa mwenye umri wa miaka 29 aliigiza na kujifanya kama mwanamke kutoka kwa sauti, kujipodoa hadi kuvaa ndipo akapata kazi kama mjakazi wa ndani, kazi ambayo ameifanya kwa miezi mitano kabla ya kuamua kufanya kitendo hicho cha unyama kwa kijana wa mwenye boma mwenye umri wa miaka 19.

Kulingana na taarifa zilizoripotiwa na blogu ya Mwebantu nchini Zambia, Mukutindwa alimdanganya kijana huyo na kumuingiza kwenye chumba chake kabla ya kujaribu kufanya unyama huo ila kijana huyo alimpiga mweleka na kumshinda nguvu kabla ya kukimbia na kuripoti kitendo hicho kwa bosi wa Mukutindwa.

“Ukweli mfupi ni kwamba kijakazi huyo kwa majina Christopher Mukutindwa ambaye ameajiriwa kama kijakazi kwa muda wa miezi mitano sasa alimwita mwathiriwa chumbani kwake. Kisha akavua kitenge alichokuwa amevaa ili apate kumtendea unyama huo na ilikuwa wakati huo ambapo mwathirika aligundua kuwa mjakazi alikuwa ni yeye na alijaribu kuhangaika, na kumlawiti, lakini aliweza kumshinda," jarida hilo lilimnukuu msemaji wa polisi.

Taarifa kama hizi mapema wiki hii zilizripotiwa nchini Kenya ambapo mwanaume mmoja ambaye amekuwa akiwalaghai wanaume wenza akijifanya mwanamke alitumbuliwa na kuanikwa hadharani kwa umma.

Kulingana na taarifa zilizofichuliwa na aliyekuwa gavana wa Nairobi MikeSonko, mwanaume huyo amekuwa akiwahadaa wanaume kuwa yeye ni mwanamke na hata kukutana nao kwa vyakula na vinywaji kutokana na umbile lake lililokuwa likimtoa kama mwanamke mrembo.