Aq9ine achoma nyeti zake kwa moto, abaki na majeraha mabaya

Alitia moto kwenye nyeti zake na kukimbia baada ya moto kushika.

Muhtasari

• Aq9ine aliamua kunyoa nywele zake za siri sio kwa wembe au mashine bali kwa moto.

Image: TIKTOK

Mwanatiktoker Aq9ine alizua gumzo mitandaoni kutokana na video yake aliyoionyesha akijaribu kuteketeza sehemu zake za siri kusambaa mitandaoni na kuzua sintofahamu.

Kijana huyo mchekeshaji ana utata kutokana na tabia ya kutengeneza video ambazo zinatisha na kuogofya.

Hivi majuzi kijana huyo kutoka Meru Aq9ine alivunja kimya kwa wanamitandao alipoamua kunyoa nywele za sehemu zake za siri sio kwa wembe au mashine bali kwa mafuta na  moto.

Kwenye video hiyo anatia sehemu za siri mafuta na kuzitia moto jambo lililosababisha moto mkubwa kuwaka zaidia ya matarajio yake.

Hilo ni mojawapo ya matukio mengi yenye utata ambayo Aq9ine ameyafanya katika siku za hivi majuzi.

Miezi kadhaa iliyopita alikuwa akivuma baada ya kutengeneza video akifanya kitendo wa kupika na kula popo.

 Baada ya kula popo mwanatiktoker huyo alianza kupatwa na magonjwa ya ngozi ya kuvimbia yaliomfanya kulazwa hospitalini kwa muda. Alifichua haya alipokuwa akihojiwa na Presenter Ali.

Alianza kujihisi kama ''anatokwa na ngozi'' kwa sababu ya kufura kwa ngozi yake baadaye akaanza kuwa na kikohozi kibaya.

Kwenye mahojiano hayo alisema, kuathirika kwa kula popo sio kumaanisha ataacha kumla mdudu hiyo.

Aq9ine bila kusikia woga alifichua kuwa anapania kuwala wanyama kama vile nyoka,nzi na konokono kwenye video zake zijazo.

 Baadaye alikanusha madai ya kuwa alikuwa amekula buibui wala sio popo kama alivyokuwa ametaja awali.

 Inaonekana Aq9ine hajawai jifunza somo lake kutokana na tabia zake za kuudhisha sababu kuu ikiwa kujaribu kuwavutia wafuasi wengi.