Kutana na mzee mwenye wake 10, watoto 98 na wajukuu 568

Mzee huyo alisema alianza kuitwa baba akiwa na umri wa miaka 17 tu na sasa ana miaka 67.

Muhtasari

• Alisema kuwa mke wake mdogo kwa jina Kikazi ni mdogo kiumri kuliko hata baadhi ya wajukuu wake.

musa Hassaji, mzee mwenye wake 10, watoto 98
musa Hassaji, mzee mwenye wake 10, watoto 98
Image: Screengrab, YouTube//Afrimax

Hadithi ya mzee mmoja kwa jina Musa Hassaji mwenye umri wa miaka 67 imekuwa gumzo la mitandaoni baada ya kudai kwamba ana wake 10 na watoto 98 wote walio hai.

Mzee huyo raia wan chi jirani ya Uganda alieleza hadithi yake katika blogu ya Afrimax kwenye YouTube na kusema kwamba anajivunia kuwa na wajukuu wapatao 568 mpaka sasa.

Wengi wamemfananisha mzee Hassaji kama baba wa Imani katika Biblia, Abraham aliyetajwa na Mungu mwenyewe kama baba wa mataifa.

Kulingana na Makala hayo, Bila shaka mzee Hassaji huenda ndiye mtu mwenye familai pana zaidi nchini Uganda, ambapo alijipiga kifua kuwa alianza kuzaa na kuitwa baba akiwa na umri wa miaka 17 tu.

Kwa hesabu ya haraka haraka, unaweza kukadiria kuwa kila mwanamke wa mzee huyo alipata watoto wapatao tisa na zaidi.

Mwanaume huyo mwenye wake wengi anaishi nyumba moja na wake zake wote lakini amejenga nyumba nyingine ndogo kwa ajili ya watoto wake karibu na eneo kubwa analomiliki.

 “Hawa watu wote unaowaona hapa ni familia yangu. Nilizaa watoto 98 na wanawake 10,” alisema kwa kujigamba.

 Baadhi ya watoto wake si watu wazima tu bali pia wameoa na kuolewa, huku wadogo wangali shuleni.

Mzee huyo alieleza kuwa kutokea kwake kuwa na wanawake wengi ni kutokana na utajiri aliokuwa nao enzi hizo.

Alieleza kuwa baada ya kuacha shule katika darasa la 6, alianza biashara ambayo ilimpa mtaji mkubwa kiasi kwamba kila boma alilokuwa akibisha kutoa posa, alikuwa anakubaliwa haraka upesi na hivyo kujipata ana wanawake wengi.

Cha kushangaza ni kwamba mzee Hassaji alisema mke wake mdogo ni mdogo mbali kiumri kuliko hata baadhi ya wajukuu wake.