Mwanamuziki Rayvanny anatamani kupendwa,wanawake wajaribu bahati yao kwake

Chapisho hilo lilipata hisia nyingi kutoka kwa baadhi ya wafuasi na mashabiki wake hasa wanawake

Muhtasari
  • Alishiriki chapisho kwenye insta stories  akimtaka mwanamke yeyote ambaye ni mzuri na yuko tayari kuwa naye aendelee na kumtongoza
Rayvanny
Image: HISANI

Mwanamuziki na Mwandishi wa nyimbo za Bongo Tanzania, Rayvanny anatafuta  kupendwa au kuwa kwenye mahaba ya mapenzi.

Alishiriki chapisho kwenye insta stories  akimtaka mwanamke yeyote ambaye ni mzuri na yuko tayari kuwa naye aendelee na kumtongoza.

Chapisho hilo lilipata hisia nyingi kutoka kwa baadhi ya wafuasi na mashabiki wake hasa wanawake ambao walionekana wakimiminika kwenye kikasha chake wakijaribu kurusha mistari kwa Mwanamuziki huyo mahiri na mtunzi wa nyimbo.

Mwanamuziki huyo amewahi kuwa katika uhusiano hapo awali. Walakini, kinyume na wengi, alichagua kwamba njia bora zaidi ya kufanya hivyo ni kuruhusu wanawake waje kwake na kujaribu kumtongoza.

Mpango wake ulizaa matunda na baadhi yao walikuwa na hamu ya mapenzi yake.

"Jamani kama unajijua ni binti mzuri na unanifaa tfadhali naomba nitongoze,"Aliandika Rayvanny.

Kama vile wanamuziki wamekuwa wakitafuta kiki ili kutoa kibao kipya, je Rayvanny anaweza kuwa anatafuta kiki, kupitia ujumbe wake wa kutongozwa?