Kuwa 'single mother' sio rahisi-Msanii Betty Bayo asema

Aliongeza nukuu akisema kuwa kuwa mama asiye na mwenzi sio rahisi kwani lazima utoe kodi ya nyumba, tokeni na bili zingine zote.

Muhtasari
  • Betty ni mama wa watoto wawili ambapo amekuwa mama asiye na mume kabla ya kukutana na mume wake wa sasa

Mwanamuziki wa nyimbo za injili za Kikuyu na gwiji wa mitandao ya kijamii Betty Bayo ambaye hayuko tayari kukengeushwa na wachochezi amesema kwamba sio rahisi mama kuwalea wanawe pekeyake.

Betty ni mama wa watoto wawili ambapo amekuwa mama asiye na mume kabla ya kukutana na mume wake wa sasa.

Saa kadhaa zilizopita, aliamua kumbariki mmoja wa akina mama wasio na waume nchini  na kipande cha ardhi kama njia ya kuwasaidia wasio na uwezo.

Alimpa kiwanja mama mmoja ambaye amekuwa mgonjwa na anayeishi katika nyumba ya kukodisha ambaye Karagu Muraya alikuwa amechapisha hadithi yake kwenye mitandao ya kijamii.

Aliongeza nukuu akisema kuwa kuwa mama asiye na mwenzi sio rahisi kwani lazima utoe kodi ya nyumba, tokeni na bili zingine zote.

Aliongeza kuwa hakuwa na mengi lakini kiwanja ambacho amemzawadia mama Laurence ilikuwa ndoto kutimia akiamini watapata pesa za kumjengea nyumba.

"Mnajua nyinyi nyotekuwa  singo mothersio rahisi ,yaani singo mum lazima ushughulikie kodi ya nyumba,kulipa stima zote ni wewe😓. Naweza kuwa sina mingi lakini kile kidogo ninacho nimebariki maisha ya mama Lawrence kipande cha ardhi hii ilikuwa ndoto imetimia na Mungu ata hio nyumba itaisha tuuKarangu Muraya wewe ni wa Nguvu," Aliandika Betty Bayo.