Wanandoa walioharibikiwa na mimba mara mbili mfululizo wapokea mapacha 3

Wanandoa hao walikuwa wanasherehekea mapacha wao 3 kufikisha miezi minne.

Muhtasari

Wanandoa hao walisema waliwapa watoto hao wao wazuri majina ya Toni, Tise na Tinde mtawalia.

Instagram
Instagram

Wanandoa ambao walipitia uchungu wa kuharibika kwa mimba mara mbili mfululizo wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kujaaliwa na watoto watatu mapacha kwa mkupuo – wavulana wawili na binti mmoja.

Wanandoa hao walisimulia hadithi hiyo yao kupitia ukurasa wao wa Instagram walipokuwa wakisherehekea watoto wao kufikisha umri wa miezi 4 tangu kuzaliwa.

Hapo awali wanandoa hao walipitia uchungu wa kuharibika kwa mimba mbili kabla ya kuwasili kwa seti ya mapacha watatu. Mama wa mapacha hao watatu, Eniola Oyinkansola, alichapisha picha za watoto hao warembo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Picha hizo nzuri ziliwekwa baadaye kwenye Instagram na @pregnancybabynyou, na Eniola na mumewe walijawa na furaha walipokuwa wakipiga picha kando ya watoto.

"Mungu aliibariki familia yangu na watoto watatu baada ya mimba kuharibika mara mbili. Ni bwana pekee ndiye awezaye kukufuta machozi, kuwa na imani, wewe unafuata," ujumbe kwenye Instagram ulikuwa wa matumai hai kweli kweli.

Mashabiki mbalimbali walioona chapisho hio walifurahia na kusema kweli Mungu ni wa miujiza na wakati wake ukifika kama maandiko matakatifu yanavyosema basi anatenda basi na kufeli.

"Amina. Hongera! Mungu Mkuu kweli. Nafurahi pamoja nao. Jina la Bwana lihimidiwe milele." mmoja alisema.

"Mungu wangu yuko kazini na ninaingia katika baraka hii kwa imani ❤️ Mungu awabariki" MyReam alisema.

Wanandoa hao walisema waliwapa watoto hao wao wazuri majina ya Toni, Tise na Tinde mtawalia.