Sarah Kabu afichua aliwahi haribikiwa na ujauzito

Zaidi ya yote Sarah amewashukuru mashabiki na wanamitandao kwa kuwa naye na kumshika mkono kila wakati.

Muhtasari
  • Aidha mwanabiashara huyo amesema kwamba anamuamini Mungu kwa miujiza nyingine licha ya kuharibikiwa naujauzito
Sarah Kabu na Simon Kabu
Sarah Kabu na Simon Kabu
Image: HISANI

Mkurugenzi wa kampuni ya usafiri Bonfire Adventure Sarh Kabu amefichua kwamba aliharibikiwa na ujauzito..

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Sarah amesema kwamba ingawa ni ngumu kutangaza haya kwa mshabiki yake imemlazimu.

Zaidi ya yote Sarah amewashukuru mashabiki na wanamitandao kwa kuwa naye na kumshika mkono kila wakati.

Aidha mwanabiashara huyo amesema kwamba anamuamini Mungu kwa miujiza nyingine licha ya kuharibikiwa naujauzito.

"Hii ni ngumu kuandika lakini wakati mwingine nilipoteza mapacha wangu mnamo Januari ๐Ÿ˜ข ninamwamini Mungu kwa muujiza mwingine siku moja. marafiki zangu maombi yanafanya kazi ๐Ÿ’ช @kabusimon Asante kwa kusimama nami katika nyakati ngumu,"Aliandika Sarah

Ufihuzi wake unajiri saa chache baada ya kufanya mahojiano na muunda muadhui Eve Mungai.

Akiwa kwenye mahojiano alifichua uhusiano wake na Daiana Marua,amabpo alipendekeza Diana mwite mwanawe Malaika.

Wakizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Bahati na mkewe hivi majuzi walifichua kwamba wangependa mapendekezo kadhaa kwa ajili ya jina la binti yao.

Afisa mkuu mtendaji wa Bonifire Adventure leo alifichulia umma kuwa yeye ndiye aliyemsaidia Diana kuchukua jina la Malaika.

"Congratulations @diana_marua and @bahatikenya ๐ŸŽŠ ๐Ÿ‘ ๐Ÿ’ team Dee finally my name won their hearts๐Ÿ† ๐Ÿ™Œ ๐Ÿ‘ baby @malaika_bahati welcome to the world ๐ŸŒŽ we love u โค๏ธ aki am getting serious baby fever๐Ÿ˜ขkaribu nikuimbie karibu kenya hakuna matata๐Ÿ˜,"Sarah Aliandika.